Mtela Mwampamba jipime!

Nadhani huyo uliyemtaja ndiye anayeongoza kuwa na Id nyingi na mleta hoja za kusifia wadosi wake. ha ha ha ha CC Jingalao
kama si ile dhambi sahv angekuwa mbunge wa mbozi
Teeeeeeeeh teeeeeeeeh teeeeeeeeeh, hiyo ndiyo dawa ya msaliti
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikisikia na kuona katika vyombo vya habari mbalimbali ukiwa unatoa matamko, kusifia na wakati fulani kukosoa vyama vya upinzani kupitia JUKWAA LA WAZALENDO!

Aidha umekuwa ukitajwa kama katibu wa jukwaa hilo. Sijawahi kusikia mwenyekiti wa jukwaa hilo, sijui kama kuna wajumbe, sifahamu kama jukwaa hilo lina uongozi kama ulivyo kwenye vyama au majukwaa mengine.

Jukwaa huru la wazalendo, mimi nina maswali yafuatayo:

1. Alianzisha nani jukwaa hilo?

2. Kwa malengo gani??

3. Lilisajiliwa lini??

4. Je, siyo jukwaa la kusaka vyeo na umaarufu ili waonekane??

5. Nani mwenyekiti wa jukwaa hili??

6. Ofisi za jukwaa hilo ziko wapi??

7. Jukwaa hilo linatusaidia vipi sisi watanzania??

8. Kwanini Mtela Mwampamba anaye dhaniwa kuusaka ukuu wa Wilaya na vyeo awe katibu mkuu wa jukwaa hilo??

9. Kwanini kinara wa matamko katika jukwaa hilo ni Mtela Mwampamba peke yake??

10. Jukwaa hilo lilifanya uchaguzi wa viongozi wake lini?? Au lina Mfumo kama wa Ccm kwenye ngazi ya uenyekiti yaani kupokezana??

"MAJUKWAA YA MATAMKO"!!

NB: Anaye fahamu na anaweza kujibu maswali haya naomba anisaidie pia kufahamu.
 
Mchumia tumbo yule kijana
Naona karata yake ya mwisho ya udcc imempita sasa anaoga kwenye maji ya kina kirefu
 
Huyu Mtela mwampamba njaa itammaliza.

Sasa hivi anaugulia maumivu ya kukosa u DC
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikisikia na kuona katika vyombo vya habari mbalimbali ukiwa unatoa matamko, kusifia na wakati fulani kukosoa vyama vya upinzani kupitia JUKWAA LA WAZALENDO!

Aidha umekuwa ukitajwa kama katibu wa jukwaa hilo. Sijawahi kusikia mwenyekiti wa jukwaa hilo, sijui kama kuna wajumbe, sifahamu kama jukwaa hilo lina uongozi kama ulivyo kwenye vyama au majukwaa mengine.

Jukwaa huru la wazalendo, mimi nina maswali yafuatayo:

1. Alianzisha nani jukwaa hilo?

2. Kwa malengo gani??

3. Lilisajiliwa lini??

4. Je, siyo jukwaa la kusaka vyeo na umaarufu ili waonekane??

5. Nani mwenyekiti wa jukwaa hili??

6. Ofisi za jukwaa hilo ziko wapi??

7. Jukwaa hilo linatusaidia vipi sisi watanzania??

8. Kwanini Mtela Mwampamba anaye dhaniwa kuusaka ukuu wa Wilaya na vyeo awe katibu mkuu wa jukwaa hilo??

9. Kwanini kinara wa matamko katika jukwaa hilo ni Mtela Mwampamba peke yake??

10. Jukwaa hilo lilifanya uchaguzi wa viongozi wake lini?? Au lina Mfumo kama wa Ccm kwenye ngazi ya uenyekiti yaani kupokezana??

"MAJUKWAA YA MATAMKO"!!

NB: Anaye fahamu na anaweza kujibu maswali haya naomba anisaidie pia kufahamu.
Nikusaidie swali no.10
Lina mfumo sawa na ile saccos yenu, mwenyekiti ni wa milele daima(mr dj)
 
Na sisi tufikishie haya maswali KWA VIJANA WA MATAMKO WA CHAMA CHENU....

1..Tokea utawala wa serikali hii mpya umeingia madarakani wameishatoa matamko mangapi...???

2..Na je ni upi utekelezaji wa hayo matamko umeisha fanywa na serikali mpka sasa......??

3..Na je,ni faida zipi chanya wamezileta kwenye jamiii juu ya hayo matamko yao mpka sasa...??

3...Na kwanini mpka sasa hatujaona utekelezaji WAO wowote wa maandamano yao NCHI NZIMA..??

4...Ni mrejesho upi wa mafanikio waliofikia mpka sasa wanaweza tupa kuhusiana na kuwabagua kwenye masuala yote ya kijamii,kiuchumii watanzania wote ambao ni wanachama na wapenzi wa CHAMA CHETU PENDWA CCM???

5..Na je ni kwanini wamekua ni BARAZA la porojo NA matamko ya matukio lakini linatokuja suala la VITENDO juu ya hayo matamko ni ZERO????

6..Je,,NI kweli haya matamko yao wamegeuza ni kama vile SACCOSS inayowaingizia posho za BURE??

NOTE:WAKUU mnaweza ongeza maswali mengine
 
Siku chache baada ya uteuzi wa wakuu wa wilaya, Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania limeeleza kufurahishwa na namna Rais John Magufuli anavyozidi kujipambanua kwa Watanzania kuwa Rais wa Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa.

Katibu wa Jukwaa hilo, Mtela Mwampamba akizungumza Dar es Salaam jana alisema uteuzi wa wakuu wa wilaya umezingatia uadilifu, uwajibikaji, uzalendo na uwezo wa kiongozi husika katika kuwaunganisha wananchi.“Jukwaa linatumia fursa hii kumpongeza Rais kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya alioufanya hivi karibuni. Rais amezidi kudhihirisha kuwa yeye ni kiongozi anayeishi na kusimamia kile anachoahidi kwa vitendo.

“Rais alisema na namnukuu; ‘Nimeona vijana ndio wachapakazi, wasiopenda rushwa na wazalendo, hivyo nitaendelea kuwaamini ndani ya serikali yangu kwa kuwateua kunisaidia kazi mbalimbali’, mwisho wa kunukuu.

“Hili amelitimiza na kulithibitisha katika uteuzi huu wa wakuu wa wilaya ambapo kwa zaidi ya asilimia 70 ya wateuliwa wote ni vijana. Sote tunajua vijana wana ari, utayari na shauku ya kuongoza kwa sifa ya kiuongozi ambazo ni uadilifu, ubunifu, uwajibikaji na uzalendo."

Alisema jukwaa hilo linatoa rai kwa Watanzania, viongozi wa dini na kisiasa kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli katika harakati za kuleta maendeleo.

SOURCE:HABARI LEO
 
Hakuna kitu hapo, ulitegemea aseme nini? Alishanyea kambi Ukawa akatimuliwa, akosoe ale wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom