Nadhani na ndivyo ilivyo kuwa kila mfanyakazi mwenye ajira rasmi analipa PAYE. Hii ni kwa hata wabunge na viongozi wengine.
Lakini ukienda mbali zaidi wabunge huwa wanamalizana na serikali baada ya utumishi wao wa miaka mitano. Hawa hawana pensheni kama rais, waziri mkuu Makamu wa rais majaji na viongozi wengine ambao wanalipwa 80% ya mshahara wa cheo kinacholingana tena kwa muda huo.
Kuna mtego ambao serikali hii isiyo sikivu imeuweka na kama utanasa basi kilio kitakuwa kikubwa sana mwaka ujao wa fedha!
Umejiuliza ni kwa nini kodi inayopendekezwa kukatwa mwaka 2020 iwasilishwe kwenye bunge la bajeti mwaka 2016? Huu ndiyo hasa mtego wenyewe.
Kwamba endapo kama serikali itafanikiwa kufyeka mafao ya mbunge mbali na ile PAYE basi itakuwa imejirahisishia njia ya kufyeka mafao ya kina kabwela na pangu pakavu wengi hapo mwakani. Kuna uwezekano mkubwa kama bunge la mwaka huu litaridhia kujilipua kwa kukubali kukatwa kodi kwenye mafao basi bunge la mwakani litakuwa na kazi rahisi ya kufyeka kodi kwenye mafao ya watumishi wengine ndani ya mifuko ya hifadhi ya jamii e. g NSSF, PSPF na mingine. Hapo ndipo mtego utakuwa umekamilika!
Sasa unajua ni kwa nini walete mwaka huu na siyo mwaka 2019? Hii ni kwa sababu watumishi wengi ni wa mikataba na hawana pensheni hivyo wengi huchukua mafao yao baada ya miaka miwili ya mikataba! Sasa kama watafanikiwa kuanza na wabunge, watakuwa wamejipa uhakika wa kuwapata wengine mwakani na hapo watakuwa wamefaidi mapema kuyakata mafao ya makabwela wengi wanaoishi maofisini kwa mikataba.
Mimi binafsi sihafiki kabisa mbunge kukatwa kodi kwenye mafao kwani haitakomea hapo! Kama serikali itafanikiwa mwaka huu, basi vile visenti vyako unavyopigia hesabu kila siku kule NSSF jiandae kulima asilimia hiyohiyo itakayolimwa kwa mbunge! Usibishe!
Aidha badala ya kuweka mtego huu wa kukata mafao ya wengi wasio na pensheni, ni vyema wakaondoa posho za bunge na kupunguza ile 80% wanayokula kina Kikwete, Mkapa, Bilal na watafunaji wengine wengi ambapo mfano; utakuta Kikwete mbali na kugharamiwa kila kitu na serikali bado anaingiza zaidi ya milioni 15 kila mwezi kama pensheni.
Hii serikali isiyo sikivu inaturudisha wapi?