Mimi kwa jinsi alivyoandika kichwa cha habari, mimi nilifikiri labda itakufa kutokana labda na SERVERS kushindwa kuaccomodate load ya taarifa, kumbe jamaa ni HATER tu ambaye yeye binafsi kuna WATU au TAARIFA hazipendi basi anaconclude ujinga au amekosa pesa ya BUNDLE ya KUPLAY Video. What a moronic mindset...
Yes inawezekana hata mimi niliwahi kuwaza hivo,itakua njema mkuuMillard kaajiri vijana ndio wanafanya kazi kwa sasa,nna hakika hao vijana ndio walikublock. Huu ujumbe nitamtumia private kwenye namba yake.
Ushauri mzuri wenye lengo la Kuboresha. Mengi uliyoongea ni kweli kabisa sababu na mimi huwa napita pita kwenye hiyo blog. Mfano front page kuna habari ya Nisha hana Mimba hii ni ya zamani sana.Define Density....
Define History....
Wakuu Mimi ni mpenzi wa mitandao ya mbali mbali ya kijamii (ya ndani ya nchi) ikiwemo baba lao JF, Millard Ayo.com, Issa Michuzi, etc.
Leo naomba nijikite kwa Millard Ayo.
Huyu bwana mdogo kwanza nampongeza sana kwa juhudi za kutumia kipaji chake vizuri katika tasnia ya habari. Nakumbuka kipindi kile miaka ya nyuma kidogo akipita mitaa yetu ya kujiachia Mwenge akienda ITV ...aisee bwana mdogo alikuwa na mapenzi na kazi yake kweli kweli.
Alitangaza vituo mbali mbali Na kipindi tofauti tofauti mpaka alivyofikia hatua ya kujikita katika kazi zake za kuendesha blog yake na TV yake ya mtandaoni (online "Ayo TV").
Aisee mwanzoni blog yake ilikuwa inajaa habari kede kede tena zilizochambuliwa kwa kina na kuandikwa vizuri sana Kiasi kwamba msomaji ukiisoma habari husika basi wewe umemaliza hata utamu wake hata gazeti au RTD habar saa mbili unatupa kule.
Ilifikia hatua mpaka ikasemekana bwana mdogo ndiye mtangazaji kijana na mwenye haiba ya kuvutia makini ya watu kwa kiasi kikubwa hapa bongo na anapiga hela ya kutosha " google addens" na matangazo ya wadhamini wake kama tigo ,GSM, NHC,NMB, etc kwa hilo nami nililiona na Nina mpongeza sana
Hakika blog yake ilitisha sana na kupendwa na Mimi na wewe unayesoma Uzi huu (kwani Nina Hakika lazima ushawahi peruzi habari kwa Millard Ayo. Com. Ni mashuhuda wa namna Dogo alivyokuwa akibamba.
Kifo cha mende kinacho mnyemelea huyu bwana mdogo na blog yake ni kama ifatavyo:
01. Kujaza ma video kibao kwa kila habari yake huku akijua fika kuwa bando la Ku download video hizo ni shida kubwa kwa watu wake wengi. Bando la kuunga unga jombaaa.
Na pia mitandao mingine network zao sio stable (more than 95% ni 3G, H,E...hapa 4G ni wa kubahatisha esp wa dar) hivyo watu wengi kuishia kusoma heading tu na kushindwa kupata kile walichokitarajia kwa kuwa video zinakuwa nzito Ku play on time na pia kuhitaji chaji ya kutosha kwa tendo hilo.
02.Kujikita kupewa habari na maripota uchwara. Zamani ulikuwa una zileta wewe mwenyewe au unatuma vijana wako wenye weredi na kazi, matokeo yake siku hizi unaokota okota tu habari za makanjanja mitandaoni na kutubandikia. Badilika na tafuta habari nzuri tena za kitaifa na kimataifa Hasa zile zenye tija, na sio kuweka breaking news za hovyo hivyo (hizo ilibidi ziwe kwenye chitchat na sio kwa kwako,
Mfano: Flora mbasha apata mchumba...aagggghhhh., wasafi walivyosherekea happybirtdhday ya chibu, shilole na snura waeleza siri ya misambwanda yao, etc
03. Kujaza habari za kina Waller na WCB utafikili watu wote tunaotembelea blog yako ni team bongo movie na team bongo fleva.
Tunapenda utuwekee habari mchanganyiko, za siasa, michezo, kimataifa na sio kujaza habari za watoto wanaoishi maisha feki tu (celebrities wengi wa bongo ni feki feki tu). Zamani ulijitahidi na kila mtu alipotembelea blog yako alifaidi habari za upande wake au azipendazo.
04. Punguza utitiri wa matangazo kwa kila habari ....yaani nusu ya blog na habari zako umejaza matangazo utafikili Yale machata walioyopaka kwenye gari la miss Tanzania Diana Eddo au ule ukuta wa EATV kwenye kipindi cha Friday night walichokuwa wanapiga chata na sahihi kila mtu Kiasi kwamba hata hujui kilichoandikwa.
05. Punguza vile vihabari unavyo okoteza blog za Nigeria na marekani. Huwa unaandika (Je wajua au Je wafahamu....) Sijui jamaa anayeendesha gari akiwa kafumba macho, mjue kimbau mbau anayetafuna Bonge nyanya la 150kg bila kuishiwa pumzi, wanawake waliovunja rekodi ya kuwa na sura ngumu, ufahamu Nyumba za gharama kubwa duniani, binadamu mwenye kucha ndefu, mtoto mwenye kitambi kuliko wote dunianj, cheki Floyd M.anavyokula bata etc
Kwa mtizamo wangu hizo ni habari za kitoto sana, weka habari za kitu uzima na sio kufanya kama blog ya watoto wa Sunday school. Angalia brother Michuzi, haweki vituko vituko vya majuu kwani vingi ni uzushi (with much more hyperboles) na kutufanya wasomaji wako kama wote ni watoto.
06. Kuwa unaondoa flont page au kwenye interface ya blog yako habari za nyuma, yaani unakuta habari inakaa zaid ya miezi 4 mfano, miss Tanzania afunguka kilichojili miss word, kila siku ipo hapo, saa hizi umeweka mume wa flora afunguka, etc yaani ina kera, kuwa kama wengine Dogo, habari ikipita ina kaa archives huko (tupa kapuni) na sio mtu anafungua mi habari la kitambo kirefu lipo tu utadhani ni current news. Za zamani atazisaka kwenye maktaba.
So make sure you update your news accordingly and with time in order to cutter the needs of your fans. Hapo uta win mdogo wangu.
Kwa leo ni hayo tu mdogo wangu Millard Ayo, nimeamua kukushauri. Yafanyie kazi blog yako itapendwa sana kama zamani ila ukipuuza blog yako inaenda kufa kifo cha mende kama zingine zilivyokufa mfano kina mpekuzi blog, etc
Kwahiyo unapaswa kujua ana MAMILIONI ya WASOMAJI tena wanaopenda INTERESTS tofauti, hivyo usitegemee kukuta TAARIFA ZINAZOKUFURAHISHA wewe tu, Yewe mwache afanye biasharaMkuu Mkaruka kutiki mkaruka...uliwoo...IJA milimo.
Mimi.ni shabiki wake sana kila siku Nina soma.magazeti yake anayo post
Kwenye twita huu uzi ungetosha?Ushauri mzuri wenye lengo la Kuboresha. Mengi uliyoongea ni kweli kabisa sababu na mimi huwa napita pita kwenye hiyo blog. Mfano front page kuna habari ya Nisha hana Mimba hii ni ya zamani sana.
Mkuu kwa sababu ushauri wako ni Positive ungecheck nae kwenye twitter yake sababu kwenye blog yake hakuna sehemu unayoweze kupost maoni ya ujumla kuhusu blog hiyo.
Sidhani labda angeandika kwa kifupi au angemcheck instagram or whatever....Kwenye twita huu uzi ungetosha?
Wahenga wanasema...."wivu ni kudonda ukishiriki utakonda"
Eti anajaza matangazo-sasa hii si ni airtime?anzisha ka blog kako kama utapata tangazo hata la duka la Mangi mtaani kwako
Kuna mtu amesema huko kuna vijana wake wao wanakupiga tofaliSidhani labda angeandika kwa kifupi au angemcheck instagram or whatever....
Msimamo wa watu wawili watatu unatosha kufanya management decision ya kibiashara aliyo complain.?Ndo Changamoto yetu sisi waswahili. Never argue with your client. Hawa wa bando la shillingi mia mia ndo wasomaji wa habari zake..leo unataka kuwadharau. Ukifanya biashara lazima uwe mwaminifu kwa wateja wako. Ujue wanataka nini na wanauwezo gani (purchasing power).
Sasa ushishangae ukiona akina Bakhresa anazidi kutajirika. Maana anajua wateja wake wanataka nini. Kama ni juice ya Azam hata ya shilingi mia tano anawatengenezea.
Know your customer. Know your audience!