Wakuu, ninaamini kila mtu amewahi kuhudhuria shule kwa njia moja au nyingine na kila mtu hapa amefundishwa na Mwalimu katika ngazi mbalimbali...kuanzia msingi, Sekondari mpaka Chuo.
Ni mwalimu yupi alikuwa msaada sana kwako hadi umefika hapo ulipo?
Mtaje na ni vyema ukasema na shule aliyokufundisha.
Mwlimu Hidden -maths
Moddy physics & Mgote -physics
Omar hakim & Mbuga - Biology
Unga & Mbuga - Chemistry
Walikuwa ni msaada mkubwa kwa wanafunzi na Bado wanaendelea kuwa msaada.
Wamenisaidia kwenda shule ya vipaji japo Sina kipaji maalumu,Ningetamani waendelee kutufundisha mpaka chuo sababu ya mazoea
NOTE:
bila kuongeza juhudi binafsi huwezi kufanikiwa.
Namkumbuka mr. Masemele mwl. Wa bookeeping pale Jitegemee! Alikuwa hachapi fimbo moja maana akaunt haita balance, ilikuwa fimbo 2,4,6 nk! Alikuwa anadai aki debit 1 lazima a credit 1 iliusitembee upande upande! Kwa kweli ilikuwa very funny.
Darasa LA 4 mwalim sirikwa mwanajeshi,,alinifanya niwe na adabu kwa wakubwa na wadogo,mwalimu mmoja muhaya Mama Lugwereka nimekosa swali LA msamiati nikapigwa fimbo 133 sitasahau