Mtaalamu wa Kenya asema biashara na China imeboresha maisha ya Waafrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,091
1,094
VCG211433578600.jpg


Biashara inayokua kati ya nchi za Afrika na China katika miaka 15 iliyopita imetumika kama kichocheo cha ajira na kuinua kiwango cha maisha katika bara la Afrika.

Katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Profesa Xn iraki wa Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya amesisitiza nafasi muhimu ya uwiano wa kibiashara kama msingi wa kunufaishana, na hivyo kuongeza kasi ya maendeleo barani Afrika na China.

Profesa Iraki amezungumzia umuhimu wa majukwaa kati ya China na nchi za Afrika, hususan Kenya, kama Baraza la Ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika (FOCAC), na kueleza nafasi yao kama njia muhimu ya kuunganisha maslahi ya pamoja, kukabiliana na changamoto za kibiashara, na kutumia fursa ambazo bado hazijatumika. Profesa huyo amependekeza uwazi kati ya wafanyabiashara ili kuendeleza kwa kina uhusiano wa kibiashara na kutafiti maeneo mapya ya kibiashara, licha ya umbali wa kijiografia kati ya China na Afrika. Profesa Iraki pia amezungumzia ahadi ya China ya kupeleka bidhaa za ubora wa juu kwa bei ya ushindani, bila ya vikwazo vya ushuru, hatua ambayo ni muhimu katika kuunda mfumo wa kiuchumi ambao ni wa uwazi zaidi na usawa.

Akizungumzia mabadiliko ya kihistoria ya biashara duniani, Profesa Iraki amepongeza ushawishi mkubwa wa China, na kutabiri mwelekeo mzuri wa biashara kati ya Kenya na China ambao msingi wake ni Kenya kukumbatia bidhaa na huduma za China, na utayari wa China wa kutengeneza bidhaa bora na za gharama nafuu.

Kuhusu uwekezaji, Profesa Iraki amesema hadhi ya China kama “kiwanda cha dunia” imevutia uwekezaji wa kigeni, ambao unachochewa na ufanisi wa mifumo yake na minyororo ya ugavi.

Akizungumzia msaada wa China kwa nchi za Afrika, Profesa Iraki amesema misaada hiyo inayotolewa na China haina masharti na inaonekana kidhahiri. Misaada hiyo inaonekana katika miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu kama barabara, reli, bandari, viwanja vya ndege na miradi ya kilimo, ikiwa ni tofauti na misaada yenye masharti inayotolewa na nchi za Magharibi.
 
Back
Top Bottom