Mtaalam wa picha za Ndege athibitisha Tanzania kununua "Terrible Teen", lakini...

Aliyeshiba amjuimwenye njaa sisi ulanga tunasafili kwakutumia matrector kutokana na barabala mbovu wao wananua ndege hivi ubaguzi utaisha link ndani ya nchi ii
 
Aliyeshiba amjuimwenye njaa sisi ulanga tunasafili kwakutumia matrector kutokana na barabala mbovu wao wananua ndege hivi ubaguzi utaisha link ndani ya nchi ii
Ninyi ndio wabaguzi...nasikia mna matreka yanawasafirisha kupitia nchi kavu kisha mnazama nayo ndani ya maji na kuibuka nayo upande wa pili. Ni nani anayefaidi manjonjo hayo ya treka kama sio ninyi watu wa ulanga!! Acheni ubaguzi (very real joke)
 
Hivi sheria ya manunuzi inasemaje kwenye taratibu za kununua mali za umma

Super hero daddy
 
Vyanzo vya kibabaishaji;

Sekunde ya kwanza anathibitisha

halafu ya pili anakana taarifa yake;

what a waste..
 
Mtaalam wa picha za ndege (Aviation Photographer) anayetumia jina la Woody Aeroimages ameithibitishia Kwanza TV kuwa ndege iliyoagizwa na Tanzania ni LN19 ambayo ni mmoja ya "Terrible Teens" kama ilivyoelezwa na mbunge Zitto Kabwe bungeni wiki iliyopita.

Kupitia mtandao wa Twitter, akaunti ya Woody Aeroimages imeweka picha ya ndege hiyo ikiwa nyeupe bila nembo na pia bila injini kuonekana.

Kufuatia swali la kuhakikisha kuwa picha hiyo ni ya ndege yenyewe iliyowekewa oda na Tanzania, Woody Aeroimages imethibitisha kuwa ni picha halisi.

Kwanza TV inaendelea kufuatilia suala hili ndani na nje ya nchi.



dfcc30f32a1c8d338ff72e9a59053d83.jpg


UPDATE: Woody Aeroimages amesisitiza kuwa kitaaluma yeye ni mpiga picha mtaalam wa ndege. Tumefanya marekebisho hayo ili kuweka habari iliyo na uhakika zaidi.
Woody Aeroimages pia ameeleza kuwa kutokana na kazi yake ana vyanzo vingi ambavyo anafanya navyo kazi kwa karibu katika makampuni ya ndege ikiwemo Boeing. Ametuhakikishia kama taarifa alizopewa na vyanzo vyake vya kuaminika zikithibitika siyo za kweli basi ataiweka wazi.

Update 2:
Woody Aeroimages amerudi na jibu muda si mrefu na kusema anarekebisha taarifa yake pamoja na kuwa awali alithibitisha kuwa Tanzania ilipata LN19. Sasa amesema amethibitisha hivi punde kutoka vyanzo vyake Boeing kuwa ni LN719
e3a2fd9f369ec2ec616364a2301776cf.jpg

Kama tulivyowaahidi tunaendelea kuwaletea habari mpya kadri tunavyovipokea.

Hizi kelele za makamanda uchwara ziliishiaga wapi? Imebaki aibu tu.
 
Jamani ndege sio kama bajaji useme unaweza kutengeneza yako na kuiingiza barabarani, ndege hadi inapewa kibali cha kuruka angani si kazi ya Magufuli, wala kununua ndege ambazo zimepigwa marufuku kuruka si mimi wala wewe anyeweza kufanya hivyo, ndege ni usafiri namba moja kwa usalama duniani, ipo hivyo kwasababu kila ndege inayoruka angani lazima iwe imepitia ukaguzi wa maana na kujiridhisha kuwa hazina tatizo na ikitokea itilafu kwa ndege moja tu ndege zote za aina hiyo hata iwe nchi gani ,zitalazimika kufanyiwa marekebisho na marekebisho hayo ndiyo uimara wa ndege hiyo. Sasa embu tuambieni hizi ndege ilinunua Tanzania peke yake na ziliruhusiwa vipi kuruka kama zilikuwa zina matatizo mnayoeleza. Kinachoonekana hapa ni baadhi ya watu kuteswa na kivuli cha Magufuli na wanaona hawawezi kufanikiwa bila kuhakksha wanaua kabisa legacy aliyoiacha ndiyo wao waweze kuchomoza na kazi hii inafanywa na Zitto na genge lake
 
Back
Top Bottom