Msimamo wa Simba uliyotolewa leo kuhusu point 3 dhidi ya Kagera Sugar

d8bda86326751a8419863660a4c4432c.jpg
 
Simba bhana, ishu ngumu hii, hawana uhakika! Nani aliwambia Fakhi alikuwa na kadi ya njano?
 
Mmezoea kuwaonea watu wa Kagera eeeh? Rambirambi zimeenda kwenye miundombinu na points nazo mnataka ziende kuwasaidia kuvuka Jangwani...aaakha, hapana.
Pamoja na kuwa sikuungi mkono kuhusu kupata point tatu kuvukia jangwani (matopeni) lakini hilo la kuwaonea Kagera kuanzia kule kwenye rambirambi limenisikitisha sana.
Na Simba akinyimwa hizo point nitajua kuwa suala la rambirambi limepewa uzito.
 
Manara ishu ni hii watanzania tunataka kujua nyie ushahidi wa kuwa Fakhi alipata kadi 3 za njano katika mechi ya A/Lion dhidi ya Kagera ni nani ??. Mleteni kwenye kamati alete video ya huo mchezo basi lakini kupiga makelele na kuhoji uhalali wa kamati ya sheria kufanya review ya rufaa ya timu ya Kagera kwamba sio halali huo ni uzezeta wa kupindukia sasa kama hiyo kamati yenu ya masaa 72 ilionekana na mapungufu na kwa nini mnaipigia sana upatu hiyo kamati ya masaa 72 au kwa vile imejaa manachama ya simba tupu ?? Mmeumbuka vibaya.
 
Kagera maskini kwanini mnaonewa sana mnapokonywa kila kitu Mara rambirambi,Mara point,shida watz wanaamini dar pekee timu za dar juzi bukoba imepata mafuriko serikali kimya,barabara ndo balaa mashimo kama makaburi,yaani sijui kagera iliikosea nini serikali?
 
Simba ni timu ya hovyo sana. Yaani Manara misuli ya koo inamtoka kujaribu kurekebisha mapungufu ya wachezaji wake uwanjani. Jamani mpira tucheze kwenye nyasi sio kwenye ndevu.

Hivi yupo mwanaume rijali hasa wa kunieleza Simba Koko waliathirika vipi kwa Kagera kumchezesha Fakhi? Maana ubishi huu ukisikika nje ya nchi kuna watakaodhani Fakhi maana yake Double
 
Kagera maskini kwanini mnaonewa sana mnapokonywa kila kitu Mara rambirambi,Mara point,shida watz wanaamini dar pekee timu za dar juzi bukoba imepata mafuriko serikali kimya,barabara ndo balaa mashimo kama makaburi,yaani sijui kagera iliikosea nini serikali?
Si ndiyo hapo mkuu, sijui kitu gani watu Kagera walikosea? Hata sipati jibu mkuu.
 
Kwani Simba mnaogopa nini, si msubiri kikao kitangaze matokeo ndo povu liwatoke.

Mnataka attention ya mashabiki wenu ili waamini kwamba mnaonewa wakati mnayajua kabisa madudu mliyofanya.
 
Anasema kwamba waamuzi hawaitwi kwenye matukio mengine kwa sababu hizo kadi kila mtu aliyepo uwanjani anaiona, ila hii ya Faki wameiona watu wawili tu.
 
Back
Top Bottom