Msichana: Acha kung'ang'ania asiyekupenda utakondesha moyo

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Habari wakuu,

Suala la mahusiano hasa kwa wasichana limekuwa na changamoto na hii imepelekea wasichana hao kumng'ang'ania mwanaume hata kama hampendi.

Hii imepelekea wasichana hao 'kujishusha thamani' na pia kukondesha mioyo yao huku wakijipa moyo sikumoja nitakuja kupendwa na kuolewa.

Tahamani yako inashuka kwakuwa unakuwa umetumika ki ngono na huyo unayemng'ang'ania na pia muda wako unaupoteza pia.

Mbaya zaidi ukija kushtuka umeshazalishwa na unabaki kukumbuka shuka kutafuta wa kuishi nae wakati kumeshakucha.

Sikia msichana acha kung'ang'ania asiyekupenda unakondesha moyo wako, Omba Mungu atakupa msaidizi wa kufanana naye.

NB: Wasichana acheni kichaa cha ndoa!
 
Sio kwa wasichana tuu, hata nyie wanaume mnatia huruma sana.
Mtu hakupendi unang'angania, unamhonga hela ukiwaza labla siku atakupenda , kumbe wapi.
Mwisho wa siku anaolewa na kadi anakupa.
Tukiwa sisi wasichana tunaendelea kubadilika , na nyie fanyeni kubadilika
 
Kuna mtu unamsema humu
 
Poleee mtoa mada..kuna kitu,sio buree.umekuja na spidi kubwa saana za kuanzisha uzi zinazo ashiria mahusiano yako yanaelekea kuvunjika ama yamesha vunjika tayar...
Njoo kwangu binti,upate pumziko murua.hakika huto jutia#
 

siku hiz tena sisi wanaume ndo tunatia huruma kuliko hata nyie, kupenda kunafanya mtu ufanye vitu vya kijinga. halafu pia wanaume wajinga mtaani wapo wengi mno hata mm niliwahi kuwa mjinga kwenye mahusiano ila now i'm wiser cute b
 
Sawa nimesikia
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…