Msaada wa Kisheria

babilas25

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
481
351
Kama kichwa cha habari hapo juu kinyosema.
Baba yangu alikua ni mtumishi wa umma tangu mwaka 1981, aliendelea na kazi mpaka June 1999 alipata barua ya uhamisho kwenda kituo kingine cha kazi, kabla ya kwenda kweny kituo chake kipya aliugua ghafla akapooza nusu ya mwili ikawa haiwezi kufanya kazi na upande wa pili ukiwa mzima pia akawa hawezi kuongea. Mama pamoja na ndgu walifanya jitihada za matibabu kwa kipindi kirefu pasipo mafanikio, katika kipindi hicho aliendelea kupata mshahara mpaka January 2001, baada ya hapo hapakua na tarifa yoyote kutoka kwa mwajiri pia hapakua na tarifa ya maendeleo ya ugonjwa iliyopelekwa kwa mwajiri. Hali ya uchumi ikawa ngumu sana ikalazimika mama aende kwa mwajiri kujua ikiwa mmewe kafukuzwa kazi kwa utoro kazini au pengine kwa sabubu nyingine yoyote Alikwenda kwa mwajiri wakatafuta file lake halukuonekana kwa kipindi cha zaidi ya miaka5 mpaka Baba anapatwa na mauti 2010 tumehangaika sana kupata tarifa zake pasipo mafanikio, tangu nikiwa mtoto mpaka leo ni mtu mzima.
Mwaka 2016 nilikwenda tena kwa mwajiri nikitaka file la marehemu baba ili nikafungue madai tulitafuta saana pasipo mafanikio kwa zaidi ya majuma mawili baadae tukalipata likiwa ndani ya bahasha tofauti na files zingine zilivyo.
Mwajiri alinipa orodha ya viambata ili nikafungue madai ya mirathi moja kati ya viambta hivyo ni salary slip yake ya mwisho. Pia nlitakiwa kujua mfuko aliokua akichangia ili madai yaelekezwe kweny mfuko husika, salary slip zilizokuepo ni 1997 1998 1999 mpaka june mwaka huo zote hizi hazikua zinaonyesha mfuko aliokua akichangia. Mwajiri alitupatia Check# tukatafute kweny mifuko ya jamii tulikwenda lakini hatukufanikiwa kupata kweny mifuko yote. Nikalazimika kwenda hazina ndogo ya mkoa nako pia hawakumtambua nikalazimika kusafri mpaka Dar hazina niliwaeleza wakaniprintia salary slip ya mwisho 2001 ikaonyesha na mfuko aluokua akichangia wakanishauri kwenda kweny mfuko husika ili nikaangalie michango yake nilikwenda lakini hapakua na mchango hata mmoja uliokua umeingia. Pia nikwenda utumishi ili nikapate tarifa zake pia hakuepo kweny mfumo wao,
Ndgu zangu wenye uelewa nisaidieni Mimi nimefukia ukomo.
Karbu kwa michango yenu na ushauri
 
Pole.
Fanya hivi: Pata uteuzi wa msimamizi wa mirathi ili utambulike kisheria toka mahakamani. Pili,nenda kwa mwajiri akupe utambulisho/vielelezo vyote alivyonavyo.Tatu hazina na mfuko watashughulikia,ukiona wanazingua nenda kwenye mamlaka ( Waziri Mkuu,Rais,Waziri wa Kazi n.k) Usikatishwe tamaa.
NB.Kulikuwa n.a. uzembe fulani tangu baba yako akiwa kazini/hai
 
Asante mkuu ntalifanyia kazi hilo
 
Hapo kuna tatizo la mwajiri aliyekuwa kamwajiri Mzee. Inaonesha alikuwa hamlipii mzee makato kwa ajili ya pensheni (withholding tax). Ki utaratibu mwajiri hapa nae alifanya kosa linalostahili adhabu. Tatizo hapa linakuja kua mzee hayupo tena, angeweza fanikiwa kumshtaki mwajiri na mwajiri angetakiwa amlipe mafao yake kulingana na mda aliofanya kazi.
Cha kufanya hapo ni kupeleka mashtaka dhidi ya mwajili, na yafanywe na anaesimamia mirethi ya mzee.
 
Asante mkuu
 
Pole sana. Huyo anatakiwa issue yake ni kufuata utarabitu wa sheria za kazi kwa watumishi wa umma ambapo atakwenda ngazi kwa ngazi mpaka kwa raisi kama suala lake lisipotatuliwa na watumishi wa ngaz za chini
 
Pole sana. Huyo anatakiwa issue yake ni kufuata utarabitu wa sheria za kazi kwa watumishi wa umma ambapo atakwenda ngazi kwa ngazi mpaka kwa raisi kama suala lake lisipotatuliwa na watumishi wa ngaz za chini
Pia jambo hili limekua la mda mrefu sasa ni miaka 7 tangu mauti yampate lakini mpaka leo halijapata ufumbuzi
 
Pia jambo hili limekua la mda mrefu sasa ni miaka 7 tangu mauti yampate lakini mpaka leo halijapata ufumbuzi
Kwanza ni nani msimamizi wa mirathi ya baba yako? Pili hiyo salary slip inaonyesha alikua akichangia mfuko gani na alikua amefikisha shingapi kwenye huo mfuko?
 
Kwanza ni nani msimamizi wa mirathi ya baba yako? Pili hiyo salary slip inaonyesha alikua akichangia mfuko gani na alikua amefikisha shingapi kwenye huo mfuko?
Mimi ndie msimamizi wa mirathi, alikua anachangia PSPF nilikwenda PSPF kujua michango yako kweny mfumo wao haionyeshi kua amewahi kuchangia kweny mfuko huo waliniambia kuwasiliana na mwajiri ili apeleke michango
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…