Pole mkuuu,kama mche Na shina kwa ujumla viko salama, na majani hayana tatizo basi hao Nni wadudu amphids au thrips ndio huwa wanashambulia Maua,hufyonza MAJI Na kula Maua hivyo Maua hukauka Na kusinyaa. Chunguza vyema fungua ua moja uone kama ndani kuna wadudu weusi hivi au funza. Tafuta DAWA zenye harufu kali kama Dume,au dimethoate,au karate, dimethe,au dume kwa kuwa hizi DAWA NI kali sumu daraja LA pili,basi kabla ya kuzipiga mwagia MAJI kwanza mengi sana shambani na spray ml 10 tu za DAWA kwa MAJI Lita 15.Puliza DAWA asubuhi sana au jioni, kila wiki puliza hizi DAWA Mara moja lakini kuepuka usugu wa wadudu spray hizi DAWA ukipishanisha Na DAWA zenye kiambata/ sumu ya profenovos au abamectin. Kila lakheri