Msaada: Mtoto kupoteza uwezo wa kuongea

Vangigula

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
844
2,717
Natumai nyote mko vyema. Moja kwa moja kwenye mada, nina mtoto wa kiume ambaye mwezi wa sita mwaka huu ametimiza miaka miwili. Stages nyingine zote kama kukaa, kutambaa, kutembea, kuanza kuota meno etc. alizipitia kwa wakati. Akiwa na around mwaka mpaka mwaka na nusu alikuwa anaweza kusema mom, dady na kutaja vitu vichache. Lakini ghafla alipoteza uwezo wa kuongea. Kwa sasa anatoa tu sauti zisizo na mpangilio wowote wa lugha. Ninaomba kwa yeyote mwenye uzoefu, anayefahamu tatizo na tiba, anayemfahamu daktari au anayeweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine, asaidie. Kwa nyumbani anaishi na kaka yake wa miaka 5, ambae anaongea vizuri tu. Tumemuanzisha pia daycare ili achangamane na watoto wenzake, amefanikiwa tu kuchangamka na kuongeza interaction, lakini suala la kuongea bado limekuwa changamoto. Msaada tafadhali
 
Mkuu Habari yako?pole sana hebu kwanza mpeleke hospitali akafanyiwe uchunguzi mdomoni mwake akitibiwa ikishindikana hajaweza kuongea hebu nitafute mimi kwa wakati wako ili nikupe dawa zangu za asili mtoto wako aweze kuongea haraka na vizuri.
 
Mpeleke hospitali kwa uchunguzi zaidi..
Pia, kuwa makini na UWEZO WAKE WA KUSIKIA, huenda tatizo hilo ndilo linapelekea yeye kutokuongea.

Nilipata tatizo kwa mtoto kama hilo.Alingalia hakuwa na tatizo lolotee.
Alikuja kuongea alipokaribia four years
 
Back
Top Bottom