Msaada: Mke wa mtu amenipenda mwenyewe

puppa

JF-Expert Member
Oct 5, 2015
379
176
Mimi ni kijana wa miaka 20 nasoma chuo cha utabibu dip in clinical medicine,madam ananifundisha somo la anatomy, ameniambia kuwa ananipenda sana ameniambia mimi ni handsome nina tabia nzuri anataka tuwe na mahusiano ya siri,mume wake ni mkuu wa chuo wa hapa ninaposoma lakini ameenda kusoma India, kitu ninachokihofia kama nikikataa anaweza kunipa supp za makusudi.

Msaada jamani wakubwa zangu
 

Oa nawe tumpende wa kwako kama ni vizuri na salama halafu uje urudishe mrejesho
 
Kwanini unataka kuharibu maisha yako kwa starehe za muda mfupi....??

Hilo jambo unalotaka au kushawishika kulifanya ni la hatari sana kuliko unavyodhani....ni jambo linaloweza kuharibu ndoto zako na mipango yako yote ya maisha yako......

Nikiwa kama kaka yako kipenzi...nakusihi na kukuasa....umuepuke na kumkimbia huyo shetani aliyekuja katika sura na umbo kama la huyo madam...
 
Do what is right.
 
Umri wako tu tatizo, jitahidi dogo hata wakwako pia atapenda wengine.
 
Kama ID yako ilivo fata ule Msemo wa "MTAKA YOTE KWA PUPA...." piga kitabu bro! Temana na wake za watu. Saiv kulikoni ukamatwe na mke wa mtu ni bora ukamatwe na nyara ya serikali....!!!
 
mke wa mtu sumu siku hizi si unajua mchezo wanaofanyiwa wanaokamatwa na wake za watu ndugu,tunza nukta yako kama mboni ya jicho wakiiongezea size tu huna maisha utatembea na pampas
 
Upele humuota asiye na kucha

mtaka nyingi na saba hupata mimgi misiba

dunia hadaa ulimwengu shujaa

asiyesikia la mkuu huvunjika guu

ngoja ngoja huumiza matumbo

Kawia ufike kijana

Natafuta shule inayofundisha ujinga

Pokea like Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…