Rafiki yangu ni mtumishi wa serikalini. Mwaka 2000 aliajiriwa kama Assistant Medical Officer, na baada ya muda alijiendeleza hadi kupata Degree ya Medicine pale Muhimbili University.
Katika kipindi chote akiwa Assistant medical Officer amekuwa akilipwa mshahara kama kawaida, na Baada ya kupata Udaktari badala ya kubadilishiwa scale ya mshahara (sijui makosa gani yalifanyika) akaanza kupata mshahara mwingine kama mtumishi mpya. Inshort, akawa anapata mishahara miwili (mshahara wa Assistant Medical Officer na pia mshahara wa Medical Officer).
Juzi kati baada ya agizo la Mhe Rais kuhusu watumishi hewa, ishu yake ikabainika na akatakiwa kurudisha mshahara wote aliokuwa akipata isivyo halali (mshahara wote wa Assistant Medical Officer) aliokuwa akiupata kinyume cha taratibu. Thanks God, amefankiwa kurudisha mpaka senti ya mwisho
SWALI/HOFU YETU:-
Baada ya kurejesha pesa hizo alizokuwa akichukua illegally, je vyombo vya dola Polisi na PCCB wanaweza kuendesha upelelezi wa jinai dhidi yake?? Na kama wataendesha jinai, watajikita katika vifungu vipi, na vya sharia ipi?
Maana tumeangalia Penal Code tunaona kuwa huyu Bwana angekuwa matatizoni iwapo asingerudisha pesa zote alizokuwa akichukua, labda kosa la kuisababishia hasara serikali lingembana. Na labda tukasema labda jinai ya wizi, ambayo nayo tunaona kama ingridients za wizi zinamkwepa.
Wajuvi wa Sheria na mambo ya utumishi karibuni