Nafikiri maumivu uliyokuwa ukipata mimba za mwanzoni, ni maumivu ambayo wanawake wengi huyahisi wiki ya kwanza ya ujauzito wakati huo yai lililorutubishwa hujishikiza kwenye mji wa mimba (uterus). Haya ya mwisho yatakuwa yamesababishwa na hali ya mimba kutishia kutoka (threatening abortion) - pale ambapo mwili hukatisha ujauzito na kusababisha hali ya kujifungua kabla ya muda na kupelekea kutoka kwa ujauzito, uterine contractions zilikufanya uhisi maumivu zaidi. Pole mkuu. Nakushauri usibebe ujauzito hadi baada ya miezi 6..kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza ujauzito ndani ya kipindi hiki.