Msaada kwa Mtaalam wa Mafao ya NSSF

bukenyaimo

Member
Oct 21, 2021
99
290
Heri ya Jumamosi Wana JF
Ninaomba msaada kwa Mtaalam anayejua Mafao ya Mfuko wa NSSF. Nina jamaa yangu alikuwa anafanya kazi Sekta Binafsi. Mkataba wake ulipomalizika,akajaza Fomu za NSSF ili alipwe Mafao yake. Kwa kuwa ni msomi wa Shahada moja,NSSF wakamlipa Fao la Kukosa Ajira kwa muda wa Miezi Sita kama Sheria yao inavyosema. Wakati akiwa kwenye harakati za kutafuta Ajira Mpya tena akienda kwenye Interview Ofisi moja Dar akapata ajali ya Bodaboda na kufariki. SWALI ni Je,ndugu zake wanatakiwa wafanye nini/wafuate utaratibu gani ili kulipwa zile Pesa zake zilizobaki NSSF??na utaratibu huo waufanye baada ya muda gani tangu kifo kilipotokea??
Msaada kwa Mtaalam anayejua mambo haya tafadhali
 
Waende mahakamani wakiwa na muhtasari wa kikao Cha familia ambacho kitamteua msimamizi wa mirathi na kuainisha warithi wa marehemu, lakini pia Kama Kuna wosia wowote wa marehemu wataenda nao, wahakikishe wamepata cheti Cha kifo kutoka RITA. Mahakamani watafungua shauri la mirathi Kisha litasikilizwa na msimamizi wa mirathi atapewa utaratibu wa kwenda mamlaka husika Kama bank, nssf, n.k kufuatilia haki za marehemu na kuzigawa kwa wahusika wa mirathi Kama familia ilivyoamua au Kama wosia unavyosema...
 
Kuhusu hints za kuandika huu muhtasari anaweza kuniona. Nina uzoefu wa jambo hili
 
Unapofungua madai kwa kawaida inatakiwa ukae muda gani ili upate pesa zako?
Kama umekamilisha kila kitu kama ifuatavyo
Unatakiwa uwe na barau ya ukomo wa ajira kutoka kwa mwajiri wako wa zamani na majina unayotumia bank yafanane na kitambulisho .
 
Heri ya Jumamosi Wana JF
Ninaomba msaada kwa Mtaalam anayejua Mafao ya Mfuko wa NSSF. Nina jamaa yangu alikuwa anafanya kazi Sekta Binafsi. Mkataba wake ulipomalizika,akajaza Fomu za NSSF ili alipwe Mafao yake. Kwa kuwa ni msomi wa Shahada moja,NSSF wakamlipa Fao la Kukosa Ajira kwa muda wa Miezi Sita kama Sheria yao inavyosema. Wakati akiwa kwenye harakati za kutafuta Ajira Mpya tena akienda kwenye Interview Ofisi moja Dar akapata ajali ya Bodaboda na kufariki. SWALI ni Je,ndugu zake wanatakiwa wafanye nini/wafuate utaratibu gani ili kulipwa zile Pesa zake zilizobaki NSSF??na utaratibu huo waufanye baada ya muda gani tangu kifo kilipotokea??
Msaada kwa Mtaalam anayejua mambo haya tafadhali
Kwanza nachofahamu ili mwanachama
apate kufungua madai yake anatakiwa akae mwezi mmoja Ili kuweza kufungua madai atatakiwa kufikia katika Ofisi za NSSF karibu nae akiwa na barua
yake inayoonesha ukosefu wa ajira au Barua ya kustaafu/ulemavu ili kupewa nyaraka nyingine zinazotakiwa kuendelea kufungua Madai.
Kwa Madai mengine kama mirathi, ujauzito, matibabu na msaada wa mazishi wahusika wanashauriwa kufika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu kwa msaada zaidi.
 
Back
Top Bottom