Msaada kuhusu mshahara kwenye interview

kulwa sholoma

Member
Mar 21, 2016
34
79
Naomba kuuliza jamani kwa mwenye majibu au uelewa wowote ule ili walau iwe msaada hata kwa wengine wasiojua.

Unapoulizwa katika interview kiwango cha mshahara unaotaka kulipia ukitaja wanakuuliza kuwa ni basic au gross? Hapo wanakuwa Wanamaanisha nini? Na je kwa mtu anayeanza kuingia kwenye ajira anatakiwa ataje ipi kati ya basic na gross katika kiwango cha mshahara alichotaja?

Ntashukuru kupata maelezo kuhusu hili wadau
 
Basic salary is the amount paid to an employee before any extras are added or taken off, such as reductions because of salary sacrifice schemes or an increase due to overtime or a bonus. Allowances, such as internet for home-based workers or contributions to phone usage, would also be added to the basic salary.

Gross salary is the term used to describe all of the money you've made while working at your job, figured before any deductions are taken for state and federal taxes, Social Security and health insurance. If you work more than one job, you'll have a gross salary amount for each one.


Salary is often loosely used to mean Net Salary. Net Salary is your take home pay and it is what you get after all statutory deductions have been made. Gross Salary is your basic salary + Additions. Basic Salary is fixed; it is an agreed amount paid regularly at a fixed date usually monthly.
 
mkuu next time jaribu kufanya utafiti kwanza then uje hapa.Kwanza kama ukigoogle utapata a lot of information kuhusu hii kitu then kuna website zinazoonyehsa unatakiwa kulipwa kiasi gani based on experience and qualification.fanya home work
 
Kama Kuna mtu kakuuliza hivyo basi atakuwa amejichanganya!

Basic salary ndio gross salary na maana yake ni Mshahara kabla ya Makato,

Mfano mtu analipwa basic salary /gross salary ya 710,000 lakini baada ya Makato ya bima ya afya, mfuko wa hifadhi ya jamii, kodi ya mshahara, na Chama cha wafanyakazi anabaki na sh 553,800

Hii inayobaki baada ya Makato inaitwa Net salary /Net pay (take home)

Hivyo, kwenye ishu ya mishahara tuna basic/gross salary (salary before deductions) na Net salary /net pay (salary after deductions ambayo ndio take home )
 
Hilo huwa ni swali la muhimu sana kulijibu katika interview. Wengi wamepigwa chini kwa kukosa maarifa ya kujibu hili;

1. Ukitaja pesa ndogo, utaonekana hujiamini & hauna uelewa wa kazi uiombayo.
2. Ukitaja pesa kubwa, utaonekana uko desperate na pesa

Pendekeza Take home yako, wao watajua watakupa basic salary ya ngapi.

Dawa ni kuchezea kati kati humo, na ujiamini na uwe tayari kutetea hoja zako.
 
kabla ya kwenda interview huwa tunafanya uchunguzi ujue watu wa level yako wanalipwa shilingi ngapi:
Mara nyingi ni Range: Na Tunataja Basic Salary kwa sababu Gross inaweka na Benefits ambazo kila kampuni inatoa kulingana na sera zake.
 
Nimewapata wadau na nashukuru sana kwa mchango wenu....mi nilijaribu kuangalia kwenye Internet Lakin nilielewa japo c sana maana ckuwa na uzoefu wa hayo.... Ni kweli tunatakiwa kujiandaa na mengi sana kabla ya interview..... Tuendelee kujuzana zaid na zaid.... MUNGU AWABARIK SANA
 
Basic ni kabla ya kukatwa wala kuongezewa kitu chochote kwenye mshahara kwa hiyo haijumlishi malipo ya overtime au bonus zozote, pia haijakatwa mapunguzo yoyote kama mifuko ya jamii etc.

Gross ni baada ya kujumlishwa kila kitu, overtime, bonus etc lakini kabla ya kukatwa chochote.

Net/Take home ni kiasi unachopata kwenye account yako ya benki mwisho wa mwezi after pilato na na wengine wote wanakuwa wameshachukua chao.
 
Kwanza inatakiwa uelewe kuwa hilo ni swali na ukikosea kulijibu jua unajipunguzia point za kufaulu interview,,
So unatakiwa ujue ni aina gani ya interview unayofanya,, may be ni serikalini ama sekta binafsi
Narudia kuwa ukiona unaulizwa kiwango cha mshahara unaotaka JUA HILO NI SWALI na lina credt zake kulingana na sekta gani unayofanya interview

Kutaja kiwango cha mshahara kinaweza kuwa ni kosa la hilo swali pia Kutaja mshahara kuna weza kuwa ni jibu la swali kulingana na set up ya mshahara wao
So kuwa makini na jua unafanya interview ya wapi
 
Mkuu mimi naona kama wewe ndo umejichanganya.Basic ni mshahara bila ongezeko lolote ila Gross ni basic+marupurupu mengine yote kulingana na sera ya fedha ya kampuni husika,overtime,housing,transport etc wakati Net salary ni mshahara baada ya makato ya kisheria(Take home)
 
Sio kweli mkuu acha kupotosha, basic na gross ni vitu viwili tofauti.
 
sasa kwenye interview ataje basic au gross! hayo yote anajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…