Adolph Jr
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 5,857
- 9,343
Nimepokea, taarifa usiku huu za rafiki yangu aliyepatwa na msiba mwishoni mwa mwaka jana na kuzika January mwaka huu.
Ni mtumishi wa serikalini kapatwa na msiba ghafla akaenda kukopa Bank ya ABC ili kumsaidia na masuala ya msiba, Tsh milioni 2 hiyo tarehe 29/12/2023.
Kaambiwa baada ya masaa 24 pesa itaingia ila hadi leo tarehe 8/01/2024 pesa hakuna na kwa taarifa ni kuwa, taarifa zake kwa mkuu wake wa kazi zimeishapita kasaini apewe mkopo ila kaambulia patupu hadi leo.
Msiba uliishaisha kwa msaada wa raia wema wakamkopesha akayamaliza huko kwao, sasa ndiyo naongea naye hapa anaomba ushauri jinsi ya kujitoa kwenye mkopo huu hewa.
Msaada kwa huyu ndugu kama ni wa kisheria ajitoe tu kwenye hili janga.