Mrisho Gambo ni wa kupambana naye, si wa kumchekea

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,733
239,338
Hii ni taarifa ninayoisambaza kwa watu wote duniani wanaopenda haki.

Majukumu ya Mkuu wa Mkoa wowote Tanzania si kutunga sheria , sasa mkikubali Gambo avunje katiba ya nchi mtakuwa mnakosea sana , huyu ni wa kupambana naye hadharani na mahakamani .

Labda watu mnasahau tu , RC ni mtu mdogo sana katika nchi hii , kukamata viongozi wa dini kwa madai ya kizushi eti ya kufanya siasa ni upuuzi wa kiwango cha juu sana na kufuru kubwa sana kwa Mungu , hata kama yeye si wa dini yao , Kwanza hizi siasa anazozisema Gambo ni zipi ?

Kama mliweza kumdhibiti RC wa DSM ( sitamtaja jina ili kutii agizo la TEF ) na kimbelembele chake , itakuwa huyu mwenye kashfa ya kutukana mwanasheria kule Korogwe ?

Dawa ya moto ni moto , msitegemee mteremko , hawa vijana wa ccm si wa kuwachekea hata kidogo , wana roho mbaya mno ! Twendeni Mahakamani .

Nakala imfikie Freeman Mbowe , Mashinji , Lissu na Kibatala.

Mungu hataniwi
 
Jpm anatakiwa apeleke kijana mwingine mchapa kazi mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya!
Dar, Mwanza, Arusha, kilimanjaro na Mbeya zitakuwa na amani zaidi.
Gambo natokea kumkubali sana huyu jamaa, vijana tunaweza!
 

Japo mnaweza kusema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuwa ana matatizo ILA na sisi pia tusisahau kujiuliza swali dogo tu kwamba je na sisi pia au wale anaowagusa huwa wanafuata taratibu na maelekezo muhimu ya Kimamlaka? Ninavyojua ni kwamba hakuna Haki bila Wajibu na isije ikawa tu sisi wenye chuki nae tunataka tu kulazimisha mambo kwa msukumo tu wa Kisiasa.

Kabla ya kumshutumu Mrisho Gambo habu na sisi pia tujitafakari je tupo sahihi kwa tunayoyatenda au tunatumika tu Kisiasa ama kwa kujua au kutokujua?

Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ana makosa au haongozi vizuri Mkoa wa Arusha japo najua kama Binadamu anaweza nae pia akawa na mapungufu yake ila nadhani Watanzania wachache sasa tumezidisha tu ' Chuki ' zetu Kwake. Iweje tumuhukumu tu leo kwa jambo hili tu la mkasa wa ajali lakini tukasahau maendeleo machache ambayo pengine ameshaanza kuyafanya kwa Mkoa na Wananchi wa Arusha?

Tuache Unafiki na Siasa zisitufanye tukawa ' Wapumbavu '.
 
nyie mbulula wa ufipa
Hebumwacheni kijana afanye yake! Mlimshindwa ndo MSUKUMA wa misungwi mtamuweza GAMBO wa ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…