Mrejesho kwa huduma mpya za uwakala kwa Benki ya NMB kupitia simu ya mkononi maarufu kama (NMB Pesa Fasta)

Rurakha

Senior Member
Oct 20, 2019
122
224
Salaam

Naomba kutoa maoni yangu kwa huduma mpya ya uwakala wa NMB maarufu kama NMB pesa fasta

Binafsi ninafanya biashara ya uwakala nina miliki mashine ya NMB kwa ofisi moja pia nilifungua biashara nyingine ya uwakala kama sehem ya kuongeza mapato knilifanikiwa kupata pos ya CRDB na nyinginezo ispokuwa NMB sikupata ispokuwa nilipewa uwakala kwa kupitia simu

Ntazungumzia NMB kiukweli tangu nimeanza kutumia uwakala huu nimebaini changamoto zifuatazo

i. Biashara ni mbaya sana wateja hawana elimu ya kutosha kuhusu sim banking na NMB wateja wake wengi ni watu wa kipato cha kati, watumishi na wazee hivyo ukiwaelimisha kuhusu NMB Pesa fasta hawaelewi kabisa kwa mfano kwa mwezi mei nimepata kamisheni ya (17000) elfu kumi na saba

2. Mfumo ni mbovu kwani mteja akitoa mfumo utatuma code hata kama salio lake halitoshi na mteja hupata ujumbe kuwa ombi la kutoa pesa limefanikiwa kiuhalisia pesa inakuwa haijatoka mpaka wakala aingize code hivyo kupelekea ugomvi baina ya wakala na mteja

3. Mfumo una limits ya kiwango cha kutoa haizidi milioni 1 hivyo mawakala tunakosa fursa ya kufanya biashara

4. Mda mwingine mfumo unachelewa kuleta ujumbe wa kukamilika kwa muamala hivyo kumlazimu mteja asubirie mda mrefu

Maoni yangu ni kwamba NMB boresheni Apps ya wakala kama wanavyofanya equity Bank mko kizamani sana na nyie ni Benki kubwa acheni ubahili tengenezeni pos wakala hashindwi kununua pos mko local sanab
 
Back
Top Bottom