Mpina: Kilo ya Mahindi ni Tsh. 600, Kilo ya Mbegu za Mahindi ni Tsh. 12,000. Waratibu wa mbegu wanatoa wapi hizi bei?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
58,878
69,569
Naungana na Mpina.Wauza mbegu wameachiwa wajipangie Mbegu Kwa bei wanayojiskia Kwa nini?

Waziri Bashe aliahidi mbele ya Rais kwamba mtatoa bei elekezi ya Mbegu Wiki Jana,mbona kuko kimya Hadi Sasa?

Kwamba niuze kilo 200 za Mahindi Ili ninunue kilo 10 za kutosha ekari Moja.Huu ni wizi Kwa kujipatia faida kubwa kinyume na inavyotakiwa.
---
Akichangia hoja Bungeni Dodoma kuhusu sualala mbegu za mahindi Luhanga Mpina anasema:

"Mbegu bora za mahindi mfuko mmoja ni shilingi 22,000 hadi shilingi 24,000 kwa maana hiyo kilo moja inauzwa shilingi 12,000, wakati huo kilo moja ya mahindi ta kawaida ni shilingi 600 kwa kilo, hivi hao wanaoratibu bei za mbegu wanazitoa wapi hizo bei?

My Take
Mpina anawashinda wengi sana kutumia uzembe wa Serikali kujipatia umaafufu wa Kisiasa kama Mtetezi wa Wanyonge wakati ni tapeli tuu.

View: https://youtu.be/iiawmhgvsWs?si=rLpJjcwmep4cLzxU
 
Kwa hiyo bei ya mbegu nayo iwe 600 per kg?

Amesahau kuwa zile zinafanyiwa 1)kuchambuliwa kupata mbegu nzuri na bora 2)dawa za kuhifadhi 3)packaging 4)marketing 5)agents1

Akili za hovyo hizi; hizo ni direct costs tu.

Unachopaswa kujua ni kuwa;
Kampuni hulima mahindi yao kwenye mashamba yao, kwa kufuata taratibu zote za kitaalam.
1. Mashamba
2. Kulima
3. Mbolea
4. Kupalizi
5. Ufuatiliaji wa kitaalam
6. Wafanyakazi

Bado kampuni itafute faida.
 
Kwa hiyo bei ya mbegu nayo iwe 600 per kg?

Amesahau kuwa zile zinafanyiwa 1)kuchambuliwa kupata mbegu nzuri na bora 2)dawa za kuhifadhi 3)packaging 4)marketing 5)agents1

Akili za hovyo hizi.
Wewe acha upunguani.Miaka yote Hadi msimu wa mwaka Jana bei ya Mbegu kilo 1 ilikuwa 6,000.Hiyo Jump ya 2 times imetoka wapi?

Kabla ya hapo kulikuwa hakuna vifungashio na dawa?
 
Labda mngetusaidia wachambuzi, hiyo kilo ya mbegu ya 22k inazalisha mahindi kiasi gani ambayo on average ni kilo ngapi.

Mpina mwanasiasa mzuri, jinsi alivyoiweka ukisoma unaweza dhani mbegu za elfu 22 zinakuzalishia 600
 
Wewe acha upunguani.Miaka yote Hadi msimu wa mwaka Jana bei ya Mbegu kilo 1 ilikuwa 6,000.Hiyo Jump ya 2 times imetoka wapi?

Kabla ya hapo kulikuwa hakuna vifungashio na dawa?
Punguani ni bibi yako.

Gharama ya sukari ya miaka ile na mwaka huu bado ni ile ile?

Kwa hiyo bei inatakiwa kubaki stagnant kwa wakati wote?

Idiot!.
 
Toa upumbavu hapa.Msimu wa mwaka Jana hapo mfuko wa kilo 2 ulikuwa sh.12,000 sawa na sh.6,000 Kwa kilo Moja.

Bei za Sasa za 24,000 Kwa mfuko wa kilo 2 zimetoka wapi?

Usilete upumbavu kwenye mambo ya msingi we fala.
Ni wapi huko wanauza bei hiyo wakati huku kwetu Songea tu nimenunua Kitale 628 ya Gobo Tsh 16500 mzee? Nimepanda last week ekari 10.

Ujuaji mwingi muda nwingine unatia aibu. Hivi anajua procedure ya kuzalisha mbegu na gharama zake? Anajua specifications za uzalishaji wa Mbegu? Maamuma kabisa huyo.
 
Attachments

  • NEW PRICE.pdf
    349.1 KB · Views: 17
Labda mngetusaidia wachambuzi, hiyo kilo ya mbegu ya 22k inazalisha mahindi kiasi gani ambayo on average ni kilo ngapi.

Mpina mwanasiasa mzuri, jinsi alivyoiweka ukisoma unaweza dhani mbegu za elfu 22 zinakuzalishia 600
Mkuu,

Ukichukua hayo mahindi ya 600 kwa kilo, kisha ukapanda utaambulia mavuno hafifu kama siyo mabua.
 
Kwa hiyo bei ya mbegu nayo iwe 600 per kg?

Amesahau kuwa zile zinafanyiwa 1)kuchambuliwa kupata mbegu nzuri na bora 2)dawa za kuhifadhi 3)packaging 4)marketing 5)agents1

Akili za hovyo hizi; hizo ni direct costs tu.

Unachopaswa kujua ni kuwa;
Kampuni hulima mahindi yao kwenye mashamba yao, kwa kufuata taratibu zote za kitaalam.
1. Mashamba
2. Kulima
3. Mbolea
4. Kupalizi
5. Ufuatiliaji wa kitaalam
6. Wafanyakazi

Bado kampuni itafute faida.
Narudia kukwambia toa upumbavu wako hapa,sisi ndio wakulima tunajua anachosema.

Nimekwambia mwaka Jana bei ya Mbegu ilikuwa 6,000 Kwa kilo,Kwa nini Sasa hivi iwe 12,000 Kwa kilo?

Wakati bei Iko nafuu hayo uliyoorodhesha yalikuwa hayafanyiki? Tena this time around mbegu nyingi inazalishwa ndani ya Nchi.

Huoni hii ni miradi ya watu inaachwa makusudi?
 
Ni wapi huko wanauza bei hiyo wakati huku kwetu Songea tu nimenunua Kitale 628 ya Gobo Tsh 13,500 mzee? Nimepanda last week ekari 10.

Ujuaji mwingi muda nwingine unatia aibu. Hivi anajua procedure ya kuzalisha mbegu na gharama zake? Anajua specifications za uzalishaji wa Mbegu? Maamuma kabisa huyo. Hiyo 12,000 ni kwa kilo 2 aache kupotosha.
Ndio maana nimeuliza wapi bei elekezi za Serikali? Na kama wametoa bei watuambie.

Ukisema ni wapi, Waziri hakuwa mjinga Aliposema watakuja na bei elekezi za mbegu baada ya Wananchi kulalamika.
 
Kwa akili za Mpina ni kuwa anatarajia kilo moja ya mahindi ya mbegu ifanane bei na kilo moja ya mahindi yaliyovunwa?

Hivi tuna wabunge wajinga kiasi hiki kweli au lengo lake ndio sijaelewa?
 
Ni wapi huko wanauza bei hiyo wakati huku kwetu Songea tu nimenunua Kitale 628 ya Gobo Tsh 16500 mzee? Nimepanda last week ekari 10.

Ujuaji mwingi muda nwingine unatia aibu. Hivi anajua procedure ya kuzalisha mbegu na gharama zake? Anajua specifications za uzalishaji wa Mbegu? Maamuma kabisa huyo.
Umemaliza mjadal
 
Back
Top Bottom