Mpenzi wangu hataki kunielewa juu ya kosa langu

koboG

JF-Expert Member
Apr 3, 2016
2,656
4,853
Ndugu zangu humu wazima? Natanguliza samahani. But nachohitaji ni ushauri.

Mimi ni kijana napitia changamoto katika mahusiano yangu kama mnavyojua mapenzi yanavyoumiza hasa pale mtu unayempenda akichokwa na tabia zako na akafanya maamuzi ya kuvunja uhusiano, na wakati bado unamuhitaji, naandika haya kwa uchungu😭😭😭

Mahusiano yetu yalianza vizuri tu na tukaenda vizuri ila shida ilianzia kwangu, nilikuwa napenda sana nimtengenezee mwenzangu wivu ili asijeniacha na kitu nilichokuwa nafanya ni kupost picha za msichana mwingine na hii nilikuwa naifanya pindi mwenzangu akinikosea ila hii tabia mwenzangu ilimkera sana but sikuweza kushtuka nikajiona niko sahihi na nimefanya hiyo tabia ya kumpost huyo msichana mwingine kwa nyakati 3 tofauti

Sasa hii ya tatu mwenzangu ameona imezidi ameamua kuniacha karibu mwezi, sasa mawasiliano yetu sio mazuri baina yangu na yeye, kinachoniuma zaidi huyo dada niliyekuwa nampost siko nae kwenye mahusiano.

Mpenzi wangu hataki kunisikia hataki kuiniona ananiona mimi muongo muongo ila baada ya mambo kuwa magumu nimeamua nimueleze ukweli wa juu ya hicho ninachokifanya cha kupost huyo dada ila mwenzangu ndio hivyo hataki kunielewa

Sababu zilizonifanya niwe nampost huyo dada ni

1. Kumtengenezea mwenzangu wivu ili asije niacha

2. Akinikosea nilikuwa nampost ili walau aniulize huyo nani ili nipate chance ya kuchat nae

Maamuzi niliyochukua ni

1. Kuomba msamaha

2. Kuonesha ushahidi kuwa huyo msichana siko nae kwenye mahusiano

3. Kukutana na mchumba wangu ambae nimemkosea ili nimuelezea A-Z kipi hasa kinanifanya nafanya hivi
ila ndo hivo mwenzangu asilimia za kuniamini zimepungua amepunguza uaminifu juu yangu

4. Nimepanga safari ya kusafiri kutoka mkoa wa Katavi hadi Dodoma ili niweze kukutana nae tuzungumze hili suala japo % za kuweza kukuta ni mdogo maana bado mwenzangu ana wasiwasi na mimi ila mimi nimeamua niende hivyo hivyo japo sijui itakuaje

Nimeamua kuondoka na kumtafuta ili nifanye suluhu japo kipato changu kidogo ila nitajibana mpaka nifike huko tujadili haya mambo

Nisaidieni mawazo na namna sahihi ya kuweza kulimaliza hili suala langu

Mwenzangu mpenzi wangu yuko humu ni member sitapenda nitaje jina lake.

Kama atasoma haya maelezo nataka ajue nampenda sana na sipendi nimpoteze❤️❤️

Napitia kipindi kigumu cha mateso makali😭😭😭😭😭 mawazo , mambo yangu hayaendi muda mwingi natumia kuwaza haya tu😭😭 kazi zimesimama nakonda na ulaji wangu umekuwa sio mzuri kabisa😭
 
Angekuwa Ni yeye anapost picture za wanaume wengine ungemuelwa? Ulikuwa unamshusha thamani, ajabu imefika zamu yako ya kushushwa thamani unalalamika. Siku zote ukidhani kwamba wewe unaweza kumfanyia mtu chochote, ujuwe na wewe unaweza kufanyiwa chochote wakati wowote.
 
Ndugu zangu humu wa zima? Natanguliza samahani. But nachohitaji ni ushauri.

Mimi ni kijana napitia changamoto katika mahusiano yangu kama mnavyojua mapenzi yanavyoumiza hasa pale mtu unayempenda akichokwa na tabia zako na akafanya maamuzi ya kuvunja uhusiano, na wakati bado unamuhitaji,
Kama tamthilia
 
Ah kumbe mwenzetu umebaahatika kuopoa mrembo wa jf...homgera sana.
Ila acha ubwege bwana unamliliaje mwanamke wakati wamejaa tele....ebu nenda kwenye ule uzi wa wanawake warembo ujione ulivyo bwege kulialia hapa kisa mwanamke wa jf
 
Ok asante kwa ushauli wako mkuu, ila ningependa unipe mbinu ya kumuelewesha huyu binti maana nampenda
 
Bila ya shaka wewe ni NATO huyo mwenza wako Russia na huyo ulokuwa unampost America halafu wewe Zelenskyy hujawacha matani mpaka sasahivi rais wa Ukrain??
Ngoja upinduliwe sasa🤣🤣
Mkuu usiseme hivo nahitaji msaada wa kimawazo
 
Angekuwa Ni yeye anapost picture za wanaume wengine ungemuelwa? Ulikuwa unamshusha thamani, ajabu imefika zamu yako ya kushushwa thamani unalalamika. Siku zote ukidhani kwamba wewe unaweza kumfanyia mtu chochote, ujuwe na wewe unaweza kufanyiwa chochote wakati wowote.
Ndiomaana nimegundua kua nilicho fanya sio sahii ila kipindi nacho fanya haya niliona niko sawa yani da Mungu anisaidie hili lipite
 
Kwanza pole kwa kuachwa,

Pili hata usiporudiwa ukipata mahusiano mengine jifunze KUJIAMINI. Kutengeneza kuonewa wivu tafsiri yake ni hujiamini kama unapendwa ndo maana ulikua unamrusha roho mwenzio.

Tatu huyo memba mwenzetu anae moyo, mgombane kidogo umpost mwanamke mwingine tena more than once aloooooo

Nne punguza utoto

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom