Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,717
- 239,305
Tulipokuwa tunaandika humu kwamba ccm inapumulia Mashine kila mahali, kuna waliotupinga, Lakini kama ilivyo ada Pembe la ng'ombe halifichiki, Mwenyekiti wa CCM aliyeko ziarani Mkoani Morogoro amejithibitishia.
Ameuona Moto wa Chadema yeye mwenyewe na amejua kwamba hatutanii, na sasa kishaelewa kwamba Viongozi wake wanampiga fix dhahiri ili waendelee kuteuliwa.
Baada ya Rais kuona Maji ya Shingo, Ameongea kiutu Uzima kwamba hayo ni matunda ya 4R, huku sisi wengine tukichekea pembeni, Maana tunafahamu kwamba hakuna cha 4R wala nini.