Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Usher-smith MD

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
9,559
12,324
Msanii wa kizazi kipya Emanuel Elibarik alimaarufu kama NEY wa mitego amekamatwa asubuhi hii huko morogoro

IMG_1917.jpg


Sehemu ya wimbo wa Ney wa Mitego:

Hivi Uhuru wa Kuongea bado upo? Siamini nchi inaendeshwa kwa kiki!
Nasikia kuna viongozi wamefoji vyeti? Wapooo! Mheshimiwa hivi unamjua Bashite kutoka Kolomije? We si Dokta wa kutumbua majipu?

We mtu gani sasa? Hutaki kushauriwa, hutaki kukosolewa? ...Naona kichaa kapewa rungu! Hahahaha.

========

Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa linamshikilia msanii Ney wa Mitego, kwa tuhuma za kutoa wimbo unaokashifu Serikali iliyopo madarakani.

UPDATE II:

Siku moja baada ya Kukamatwa kwake, Rais Magufuli ameagizwa Ney wa Mitego aachiliwe na Nyimbo yake ipigwe katika vituo vyote vya Radio na TV. Kwa habari zaidi soma=>Rais Magufuli aamuru Ney wa Mitego aachiwe huru na wimbo wake upigwe vituo vyote redio na TV
 
Back
Top Bottom