Mohammed Ali wa Jicho Pevu atangaza kujiuzulu uanahabari, kuwania ubunge Nyali kwa tiketi ya ODM

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Wote waliokuwa wanapandwa na taharuki kila mara wakati Mwanahabari Mpekuzi wa runinga ya KTN Bw. Mohamed Ali kwa kuandaa makala yake, sasa wanaweza wakatuliza nyoyo zao.

Hasa watakaopumua kwa urahisi ni viongozi ndani ya Serikali ambao kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakipokezana uchungu wa mijeledi ya maneno kwa makala ya Bw. Ali.

Kisa na maana.? Bw. Ali anayefahamika kwa makala yake ya Jicho Pevu ametangaza kujiuzulu kutoka taaluma ya kufichua maovu ya kiutawala na katika jamii, yaani uanahabari na kujiunga na siasa.

Ali katika mtandao wake wa Twitter amesema kuwa "Kwa miaka 10 mfululizo nimekuwa nikisimama nanyi kuzidisha sauti zenu za kuangaishwa. Sasa ni wakati wangu wa kuwauliza, msimame nami katika harakati zangu za kuwania ubunge wa Nyali kwa tiketi ya ODM".

Ameahidi kuwa akitimiza ndoto hiyo atakuwa mshirikishi mkuu wa utawala wa haki kwa Wakenya wote bila ubaguzi.

"Ingawa utawala wa haki na maadili umeonekana wazi kuhepa waheshimiwa bungeni, tusaidiane mimi niirejeshe haki hiyo ndani ya Bunge letu", alisema.

Huku hadi sasa akiwa amebaki katika orodha ya waajiriwa wa KTN kama mhariri wa upekuzi, habari zinasema kuwa Ali hajaonekana kazini kwa wiki moja mfululizo, sasa ameonekana katika jumba la Orange House Jijini Nairobi akikimbizana na mikakati ya uwaniaji.

Wadhifa anaoulenga kwa sasa unashikiliwa na Bw Hezron Awiti, aliye na uwezo wa kuandaa kampeni kali katika kutetea wadhifa huo tena katika uchaguzi mkuu Agosti 8, 2017.

Huku kukiwa na idadi kubwa ya wanahabari ambao wanatoka taaluma hiyo na kujiunga na siasa, Ali atahitaji kila lenye kufaa katika kumenyana na Bw Awiti na wapinzani wengine.
 
Kiukweli huyu jamaa tangu nimjue ameniteka sana kwa makali zake zisizo na chembe ya uoga. Mohammed Alli ni wa kipekee sana kwa kweli
 
Jamaa alinivutia kuwa mwanahabari...Ingawa sikusomea uandishi wa habari lakini nilifanikiwa kufanya anachokifanya.
Hongera sana mkuu.. yaani mpaka ile hamu ya kuwa mwandishi wa habari inavutia kwa ajili ya huyu Mohamed Ali...!
 
Hongera sana mkuu.. yaani mpaka ile hamu ya kuwa mwandishi wa habari inavutia kwa ajili ya huyu Mohamed Ali...!
Issue ni kwamba makala zinakataliwa kwenye vyombo vya habari naishia kuziangalia mwenyewe, ila nina mpango wa kuingia kwenye nchi zenye vita kuandaa makala ambazo nitajua cha kufanya watu wazione.
 
Ulichofanya wewe Mkuu kinaweza kuonekana kwetu?
Kwa nchi hii labda nianzishe TV yangu wenye vyombo vya habari hawataki si awamu ile wala hii na sheria yetu pendwa ya habari mhhh.... Naingia Sudan na Somalia kuandaa vitu vipya..
 
Kitu chochote Ukiamua kukifanya kwa bidii na haki kisha ukikipenda kiukweli kinakutoa,Hata ukiamua kuuza nazi au vitumbua,ukiheshimu unachokifanya utafika mbali,Huyu jamaa alijijengea jina kubwa katika tasnia ya habar naweza kusema Afrika mashariki yote,Akiamua kuifuatilia habari hata kama ingekuwa inamuhusu nani,ataweka kila kitu bayana bila kukwepesha,All the best Mr Alli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…