Mnyonge mnyongeni ya mitandao ya simu

deonova

JF-Expert Member
Apr 22, 2013
742
419
Hi Comrades,

Nataka kuleta challenge kidogo hapa, wengi wetu mtakubaliana nami kuwa kupiga simu kwenda mtandao tofauti na unaotumia ni gharama kubwa sana, mfano kupiga simu za ndani ya mtandao fulani kwa bei ya sasa baada ya bajeti ya serikali ya July mwaka huu 2013 ni tsh. 5.04 kwa sekunde, kupiga nje ya mtandao (mitandao mingine) ni tsh. 7.0 kwa sekunde. Ila sasa nafikiri kwa hizi huduma za sijui Cheka Bombastik (voda), Kabang (tigo), Yatosha (airtel) n.k walau zinaokoa sana na naona sasa mtu wa airtel ananipigia kwenye line ya voda na anaongea kwa pozi zote tofauti na mwanzo ambapo mtu anapiga anakimbizana na airtime, tuseme kuanzia mwaka jana kurudi nyuma hata unapotaka kusevu namba ya mtu ulikuwa unamuuliza kwanza ya mtandao gani? Na kama ni mtandao tofauti na anaotumia yeye utakuwa unaambulia "please call me, Message na kubeep" tu, kupigiana sahau.
Sina nia ya kufanya promo yoyote hapa ila nataka kusema kuwa huu utaratibu wa promotions & offers za mitandao (kama cheka bombastic, yatosha, kabang n.k) ni mwanzo mzuri wa kule tunakotaka kufika kulingana na maagizo ya TCRA kuwa tufike mahali tuwe na gharama moja ya kupiga simu mitandao yote bila kujalisha unapiga ndani au nje ya mtandao wako.
Na changamoto nyingine nnayotaka kuibua ni kwamba sio tu iwe bei moja bali iwe ya chini as much as possible. Maana unaweza kuambiwa sawa si unataka bei moja kwa mitandao yote (on-net & off-net)? basi ni Tsh. 8.05/sek kitu ambacho bado itakuwa tatizo maana hapo hata simu za ndani ya mtandao utapiga kwa bei kubwa tofauti ya awali. Tunachotaka sio tu iwe "one price for all nets" bali iwe "one low price for all nets" TCRA najua hilo wanaliweza na liko ndani ya uwezo wao pamoja na Wizara ya Sayansi, Taknolojia na Mawasiliano.

Nawasilisha.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom