Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 14,997
- 31,279
đź“šKOMBA(BUSH BABY) Ni mnyama jamii ya kima ambaye Ni mdogo kuliko wote ambaye anatembea usiku tu mchana analala (night monkey).Bush baby Ni Aina pekee ya kima ambaye muda mwingi wa Maisha yake anatumia akiwa juu ya mti.Bush baby Ana macho makubwa yanayomsaidia kuona wadudu gizani na masikio makubwa yanayomsaidia kusikia vizuri.Bush baby ana umbo dogo Ila analia sauti kubwa inayofanana na ya mtoto,pia ana vidole vitano na kucha Kama za mtoto mdogo hiyo ndio sababu wanamuita Bush baby yaani mtoto wa porini.Chakula chake Ni matunda na wadudu lakini maajabu anakunywa pombe ya mnazi maarufu Kama tembo.Usiku anapopanda juu ya mnazi na kukuta kopo la mgema alilokinga tembo lazima ainywe.akilewa anaanguka kutoka juu ya mnazi Hadi chini au mgema anamkuta juu ya mnazi kalewa kashindwa kuondoka.Bush baby anakufa akiwa juu ya mti kamwe huwezi kumuona kafia ardhini labda awe amegongwa au kapigwa.Bush baby anaishi miaka 3 Hadi 4