Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,713
- 13,464
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvus Mrindoko amewataka wanunuzi wa zao la Pamba kuhakikisha wanalipa pesa za wakulima kwa wakati ili kuwafanya wakulima wa zao la pamba kutokata tamaa ya kulima zao hilo.
Mrindoko ameyasema hayo wakati akizindua msimu mpya wa mauzo ya zao la Pamba katika Kijiji cha Makongoro kilichopo Kata ya Magamba, Manispaa ya Mpanda huku Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Katavi, Nehemoa James akitaja matarajio ya mkoa katika zao hilo ambayo ni Kilogram Milioni 26 lakini kwa msimu huu wamefikia Milioni 12 za uzalishaji.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Filbert Bugeraha amesema bodi itaendelea kuhakikisha wakulima wanafikiwa na pembejeo kwa wakati sahihi huku mkurugenzi wa kiwanda cha kusindika pamba NGS, Njali Silange akiwahakikishia wakulima kulipwa kwa wakati.