Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mama Mghwira awasili Ofisini kwake, kuanza kazi leo rasmi

Karibu mama... Utuletee maendeleo.... Ndiyo hasa kilichokuleta
 
Karibu kilimanjaro ....Watu wa hapo ni wakarimu sana ....

Ila usiweke uvyama mbele katika kuwatawala ,ukitaka amani baki na chama chako na waache wao na chama chao ...

Ndio maana wakuu wa mikoa waliopita kama ladislaus gama na meck sadick hawakupata tabu kufanya nao kazi
 
Mungu ampe hekima na ujasiri wa kukataa maovu ya ccm. Sijui kama atapingana na mwajiri wake!.

Kafurahia uteuzi, lakini anavita kali.

ACT wamemvua uenyekiti, yeye anasema bado mwenyekiti.

Anatangaza watu wasimfuate ofisni kumwambia habari za aCT wazalendo as if anajua changamoto ziatakazojitokeza katika eneo lake.

Kiongozi huwezi kubashiri nature ya changamoto utakazokutana nazo hasa kama unashughulika na binadamu.

Ninahisi kama CCM walioachwa wakati walilia utemi kiasi cha kulazimisha ushindi kwa magoli ya mikono, asishangae wakimpiga vita mpaka basi.

Na asije akanyea kambi kwa kuwa, mwisho wake naouna kama atakosa jina katika vitabu vyote viwili!.

Anahitaji kuwa makini!
 
Aanze na kutembelea wafiwa kwa Marehemu Ndesamburo, itamjenga sana.
Kwa lugha nyepesi aanze kwa kwenda kuzoa mavi aliyokunya Mrisho pale msibani nyumbani na pale uwanja wa majengo alipoenda kuzozana na viongozi kupelekea wananchi kumkimbiza kwa zomea zomea na kufanya askari wazikoki SMG zao....akaishia kususa na kupost picha akiwa business class wakati wenzie wako msibani
 
Aende kufanya kazi yake, aachane na kwenda kutafuta visirani, hili ni funzo kwa wakuu waliopo waache kiki za kijinga ni dhahiri hata mkuu hazimfurahishi, upuuzi wa Gambo na Makonda ndio umeganya Kippi warioba asipande cheo, wajitahmini maana hata Muhongo ni rafiki sana na mkuu.
 
Karibu sana kilimanjaro mama mughwira......

Tunachohitaji wana kilimanjaro ni maendeleo kwa kasi kabisa. Siasa za visasi tunaimani hazitapewa nafasi kilimanjaro. Maendeleo hayana vyama wala imani cha muhimu tushikamane wote na hilo sina shaka na wewe hata kidogo.

Ombi langu kwako simamia kikamilifu utunzaji mazingira kilimanjaro kama alivyofanya mh. Gama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…