Mkuu wa Mkoa Dar na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni tuko chini ya miguu yenu tunawaomba mtusaidie

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Mkuu wa Mkoa na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni tuko chini ya miguu yenu. Sisi wafanyabiashara wa Mwenge tunawaomba sana sana tuko chini ya miguu yenu tunaomba mtusaidie kero ya magari, ili tuweze kupaki magari yetu kwa amani kama ilivyokuwa mwanzoni.

Waheshimiwa sisi tunatekeleza sera za Serikali ya awamu ya tano kwa vitendo, tumejiajiri, tumeajiri na tunalipa kodi. Tunalipia leseni na tunaheshimu Serikali yetu.

Hali ni ngumu sana toka kumetokea katazo la kutokupaki magari kwenye barabara ya Mwenge. Biashara zetu zinazidi kudorora.

Waheshimiwa sana, sisi ni watanzania tunaowaheshimu sana, tunawaombeni sana mtusaidie tuweze kufanya biashara. Kama kuna kosa tulilowafanyia, tunaomba mtusamehe!
 
Pole Mkuu umeandika kwa uchungu. Hata hivyo ujumbe umeeleweka na kwa heshima ya jukwaa hili ujumbe utafika kwa wahusika
 
Unachosema ni kweli!

Leo nilikuwa Napita Buguruni pale sokoni nikaona Mikungu ya ndizi Mizuri tu nikavutiwa nayo na kwa kuwa pale Hakuna Maegesho nikaona ni park katikati ya Barabara pale kwny Kama tuta la kutenganisha Barabara lakin nikaja kuambiwa ni Marufuku, nikashindwa kufanya Manunuzi niliyokusudia


sasa Soko kubwa Kama lile kukosa Maegesho hata ya Baiskeli si Upunguani?
 
Kitendo cha magari kukatazwa kupaki hapa mwenge kumeongeza mianya ya rushwa kufa kufaana
 
Mnchotakiwa kufanya ni kuita press muhakikishe makamera ya tv zote yapo,halafu mumuombe msaada Mtukufu.
Anavyopenda sifa chap chap atawakubalia
 
Hivi maigizo ya kupanda daladala na kula kwa Mama lishe kwa mgombea wa chadema 2015 iliishia wapi?
 
Tatizo ni kwamba wakati wakati TRA wanataka kodi, huku mamlaka nyingine zinaharibia watu biashara zao. Yaani hakuna common strategic goal.
 
tatizo mamlaka inayokusanya ushuru wa maegesho na TRA ni tofauti kuanzia kiitikadi mpaka kimalengo - huku ukawa kule CCM-TRA na hakuna mtu wa kuwakalisha pamoja wakawa na malengo yanayoshibishana - complementing goals
 
Jikusanyeni mfanye maombi Mungu tu ndo atawasaidia kuwalainisha watawala kuweza kuwasikiliza. Ombeni nanyi mtapewa,bisheni nanyi mtafunguliwa...... hayo ndo maoni yangu kwa sababu mwanadamu bila kuguswa na Muumba wake hawezi kukusikiliza wala kukusaidia.
Tuache kukulalamika maombi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…