Mkutano wa Wauza Simu na TCRA chini ya Makonda na Meya waisha kwa makubaliano

Kwa hiyo wanazima au hawazimi? Wanazima Leo au wamesogeza mbele ? Hiyo mikwara ni Kama hawazimi maana Kama simu haikamati network mteja si ataona wAkati wa kununua? Any way UVUMILIVU wao usichukuliwa kuwa ni incompetence
Kama kuna simu kimeo wazime tu
 
Makonda ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Meya wa jiji la Dar es Salaam.

Mafundi na wauza simu walioitwa ni wa Dar es Salaam.

Swali ni je, maazimio hayo yanawakilisha mawazo ya wauzaji na mafundi simu wote wa Tanzania au Taifa zima?
tatizo ni barabara na si dereva wa gari.
 
yaani hapa ilikuwa ni full mkwala kwa mafundi simu kwani ndio wanauwezo wakuibadili kusoma kama original, mwanzani walijisahau baada ya makala ya wadau mbali mbali kuwa mafundi wanaweza kuzihalalisha ndio wakawahi kupiga mkwala wa vyeti pamoja na kutobadili mwonekanao wa simu na utambulisho yaani imei
Hapo ndo sass wamewafungua macho watanzania na hakuna simu ya mtu wa mjini itashindwa kufanya kazi
 
Ni kama vile kuna mwanafunzi aliasafiri na kuwaacha wenzie darasa la pili sasa karejea baada ya miaka mitano anawakuta wenzie darasa la saba alafu analazimisha wote waendelee na masomo ya darasa la tatu!
Wanavyosimamia utadhani tunafungua kiwanda cha simu Tanzania.
 
Mkuu, sipingani na maazimio yenu. Ninyi mmefanya kwa sehemu yenu. Ni jambo jema.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anapokuwa msemaji wa Wakuu wote wa Mikoa Tanzania kwa jambo hili la kitaifa ninaona

kupwaya kwa dhana nzima ya uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility).
Kweli kabisa
 
Hapo ndo sass wamewafungua macho watanzania na hakuna simu ya mtu wa mjini itashindwa kufanya kazi
mafundi wote kwa kauli moja wameapishwa kutofanya bishara ya kubadili IMEI no pia kutoa msaada wowote kwa waliofungiwa.
 
Mwanzo mzuri huu,, pia kuna Radio, Tv,, Bulb,, Matairi Feki,, zoezi lihamie huko sasa .
wanakwenda na kimoja kimoja watafika tu, kwa kweli nami nawasupport TCRA kwa kuwa wateja wengi wa simu walikuwa wameanza kuwa na dharau eti ikifa hii si nachukua nyingine, sasa original bora inaanzia laki mbili, nafikiri hazitatupwa, na kuanzia hapo mafundi uchwara wote wa vibarazani watafurushwa na kwenda kusomea, sio uharifu waliokuwa wanaufanya, na kufanya mafundi simu wema na wazuri waonekane kwa mkumbo kuwa mafundi hawaaminiki.
 
Huyo hakosagi kwenye shughuli yoyote umuite husimuite yupo tu

Usiwakumbushe watu machungu ya aliyetutangulia mbele ya haki: Mzee Kabwe aliyekuwa Mkurugenzi Jiji la Dar.

Kabla ya kifo akaitwa majina yote mabaya. Siku ya msiba wake akapewa majina yote mazuri akiitwa mzalendo wa tangu enzi za Nyerere...
 
wanakwenda na kimoja kimoja watafika tu, kwa kweli nami nawasupport TCRA kwa kuwa wateja wengi wa simu walikuwa wameanza kuwa na dharau eti ikifa hii si nachukua nyingine, sasa original bora inaanzia laki mbili, nafikiri hazitatupwa, na kuanzia hapo mafundi uchwara wote wa vibarazani watafurushwa na kwenda kusomea, sio uharifu waliokuwa wanaufanya, na kufanya mafundi simu wema na wazuri waonekane kwa mkumbo kuwa mafundi hawaaminiki.
Zoezi hili litawaumiza wale wenye kipato cha chini vinginevyo what is laki mbili?
 
Back
Top Bottom