Mkutano wa kupinga rushwa London

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
7,420
7,079
Ni ukweli usiopingika kuwa dunia hasa Uingereza inapinga kwa kauli moja RUSHWA na ndio maana kama Taifa tumealikwa huko London kwenye mkutano wa kupiga vita MLUNGULA.
** Vipi Tanzania tumepewa nafasi ya kuhutubia? na kueleza mafanikio yetu kwenye kupinga Rushwa?
 
Ndio huo mkutano Mkuu wa Nchi aliomtuma Waziri mkuu?
Naamini tutapewa nafasi ya kuongea machache na bila shaka tutawaeleza jinsi tunavyominya majipu.
 
Nimesikitika wanaharakati wetu kwenye NGOs/CBOs wapo kimya kwenye vita dhidi ya UFISADI inaumiza sana hivi watanzania mbona tumepoa sana. Yaani wapinzani bungeni jii/wanaharakati jiii. Ni hatari kwa afya ya taifa
 
Huo mkutano ni upuuzi mtupu na hata mwaliko wetu huko ni kiini macho na utoto mtupu...kama huamini angalia ishu ya Panama papers itakavyoendeshwa
 
Hapo yule jamaa yetu angekaa huko wiki 3 angewatafuta mpaka dayaspora achonge nao
 
Grupu za wana-dayaspora zimepwaya ghafla chezea katapila
 
Nimesikitika wanaharakati wetu kwenye NGOs/CBOs wapo kimya kwenye vita dhidi ya UFISADI inaumiza sana hivi watanzania mbona tumepoa sana. Yaani wapinzani bungeni jii/wanaharakati jiii. Ni hatari kwa afya ya taifa
Mkuu unaweza kukikimbiza/kupigana kivuli chako mpaka ukitoe roho?
 
Nilitegemea wale wanaharakati wa enzi za uchaguzi wanahojiwa na ITV sasa ndo wangekuwa moto moto kuwaumbua viongozi wanaowalinda Watumishi hewa, lakini huwasikii popote. Daah!
 
Huo mkutano ni upuuzi mtupu na hata mwaliko wetu huko ni kiini macho na utoto mtupu...kama huamini angalia ishu ya Panama papers itakavyoendeshwa

Na ndio maana JPM kuamua kuenda kumshangilia Babu Museveni kwa kuendelea kuwapiga bao Waganda na ujanja wao wote, hakuna kitu pale, wanapoteza muda, pesa zilizochotwa zitabaki kule, yataanza mamilolongo ya sheria na haki za binadamu, mpaka wajukuu zetu wanapata wajukuu zile pesa zitakuwa kule mkuu, amini usiamini..
 
JPM asingeweza kuacha kwenda UG... pamoja na sherehe kushukuru kupewa mradi wa bomba la gesi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…