Mkutano wa jana kuhusu madawa ya kulevya uliandaliwa na nani??

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,119
Kuna mambo kadhaa kila nikayatafakari nakosa majibu yake. Yaani ni kama mpira sijui wapi juu wap chini!

Naomba kujua, mkutano wa jana uliowakutanisha Makonda na mkuu wa kitengo cha madawa ya kulevya ni nani aliye uandaaa??

Yaani uwepo wa Makonda na viongoz wengine wa kiserikali unakosa maana na majibu yake. Kama uliandaliwa na Makonda iweje makonda ndio amkabidhi mkuu wa kitengo majina ili hali wakubwa zake wapo yaani Waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani ?

Kitendo cha mkuu wa mkoa kumkabidhi majina mkuu huyo ni kama yeye ndio boss wake. Na sasa anampa majukumu. Kwa lugha nyingine ni kama anampa hadidu rejea , na inabidi afanyie kaz na mrejesho urudi kwa aliyemkabidhi!! Atampelekeaje waziri mkuu au mambo ya ndani wakati hawakumkabidhi wao??

Iwe uliandaliwa na serikali. Iweje wakuu wa kitengo hicho wakosekane kwenye mkutano huo na kumtuma Makonda. Anahusika vipi Makonda wakati hata sio mjumbe wa kitengo hicho?? Sio tu ujumbe hata hayuko chini yao kabisa!! Sitaki kuamini kwamba Makonda kachukua majukumu ya watu wengine na kujivika yeye!! Je mkuu wa kitengo hicho atakua anaripoti kwa mkuu wa mkoa??

Je maneno yanayosambaa mtaani kwamba Makonda kwa sasa kawa wa pili katika serikali hii yanaweza kuwa ya kweli?? Hii sio ya kufumbia macho ipo siku itavuruga serikali maana wataanza kutegea wakisubili yule kimbelembele ndio afanye!!

Sitaki kuamini kwamba kwa sasa serikali iko hivi.

Mkuu wa kaya!
Makonda
Makamu
Waziri mkuu
____
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…