Mkurugenzi Lushoto azuia shule zote zisifungwe muhula wa kwanza

Opera Min

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
901
658
Katika hali ya kushangaza na hulka za wateule wa Magufuli kujiamria mambo pasipo na weledi Mkurugenzi wa halmashauri ya Lushoto bwana Makwega Kazimbaya ameziua shule zote za msingi na sekondari zisifungwe kwa muhula huu wa kwanza unaoishia mwezi june 2 na hakuna kwenda likizo kwa walimu na wanafunzi wote wabaki shuleni.

Hali hii ni kukiuka utaratibu wa kitaaluma kwamba mihula imewekwa na wataalam ili kuwapa nafasi wanafunzi kupumzika kila wamalizapo nusu muhula na muhula.

Jana tulikua na kikao cha wakuu wa shule na Mkurugenzi, tulibaki midomo wazi kwa ubabe anao utumia huyu jamaa na inaonyesha kabisa anatumia ubabe mwingi kukandamiza watumishi wa halmashauri ya Lushoto. Waziri wa elimu ingilia kati jambo hili la sivyo litachochea vinyongo(ambavyo bado watu wanavyo) na migomo baridi itakayowaumiza watoto wa watu ambao kimsingi hawana hatia.

Chanzo: Ni mimi mwenyewe jana nilihudhuria kikao ukumbi wa halmashauri.
 
Usije Ukategemea Jipya Zaidi Kwenye Kijani
Sasa Elimu Imeingiliwa Yaani Kila Mtu Mjuzi
Duh!! Anajitambua Kweli Ama Anataka Fenti Feji (Front Page)
 
Duuh hii bab kubwa
 
Acha uongo mkuu. Hakuna kitu kama hiko.
Mkuu, usiwe mbishi hizi habari ni za kweli, wakuu wa shule wamepewa agizo mbali na hili mkurugenzi ameenda mbali kwa kuwaagiza wakuu wajiandae kuwapokea form six leavers wa masomo ya sayansi kwenda kufundisha kukabiliana na tatizo la upungufu wa walimu.
Nchi hii ina viroja sana
 
na nyie walimu mmekaa tuu mmeshindwa kumpinga kwa hoja mnakimbilia kulalamika JF na bado unasema eti mlikaa kikao acheni kubuluzwaa nyie; mpaka lini?
 
Ana elimu gani hiyo mkurugenzi?

Au ndio wale UVCCM walioteuliwa na kupewa madaraka yaliyowazidi uwezo?

Bila shaka huyo atakuwa na undugu na Mwakichungwa.
 
Bado subirini amri ya kulala na wenzi wenu mara 2 kwa wiki.!
Hapa kazi tuu.
 
km atawalipa nje ya mshahara sawa. lakini nje ya hapo ni ubatili na haipo kisheria
 
kisheria mtumishi ukimzuia kwenda likizo unatakiwa kumlipa basic salary ya mwezi huo.Yuko tayari au ameropoka tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…