Mkurugenzi jiji la Arusha azima hujuma dhidi ya Rais Magufuli kwa kuwatoza ushuru wafanyabiashara

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu
Kutoka Arusha

Wafanyabiashara ndogo ndogo hapa nchini kwa muda mrefu wamekuwa wakinyanyasika na askari wa jeshi la akiba 'Mgambo' ambao wamekuwa wakitumika katika halmashauri mbalimbali kwa ajili ya kuendesha operesheni za ukusanyaji mapato au usafi.

Ilikuwa ni kawaida kusikia muuza matunda, mbogamboga, chakula au machinga vitu au bidhaa zake zimechukuliwa au zimeharibiwa vibaya kiasi cha kupata hasara au kutakiwa kwenda kulipa faini kubwa ndio arejeshewe huku akiwa bado hajui atakwenda kuuza wapi biashara yake...kiukweli walipata tabu sana huku wakiwa wanategemea kuhudumia familia zao kwa kazi hii.

Mwenyezi Mungu hamtupi mja wake kwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hapa nchini alimuinua mwanaume mmoja kutoka familia ya mkulima wa pamba, ufugaji na uvuvi aitwaye Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania. Mhe Magufuli alitamka wakati anaomba nafasi hiyo kuwa hatakubali kamwe kuona wafanyabiashara wadogo wakinyanyasika.

Katika kutekeleza hili akaja na utaratibu wa kuwatambua wafanyabiashara wadogo ambapo ni wale wote ambao mtaji wao hauzidi shilingi milioni nne za kitanzania kwa kuwapa kitambulisho kwa gharama ya shilingi elfu ishirini tu kwa mwaka mzima.

Mhe Rais Magufuli akaagiza halmashauri zote hapa nchini pamoja na mamlaka ya mapato TRA kutowabugudhi au kuwafuatafuata wafanyabiashara wadogo wenye vitambulisho hivyo.

Ikiwa inaonekana wapo ambao kwa makusudi wanakwamisha nia njema ya Mhe Rais mfano mkuu wa soko kuu jiji la Arusha Ndugu Yusuph Ngenya alijirekodi video iliyomuonesha akiwalazimisha wafanyabiashara wadogo wa matunda na mbogamboga katika jiji hilo ambao wana vitambulisho vilivyotolewa na ofisi ya Rais kuwatambua wamlipe ushuru wa shilingi mia tano ambapo walimkatalia. Baada ya kukataliwa kwa madai mpaka wasikie tangazo kupitia vyombo vya habari au vipaza sauti vikipita aliwahadaa kwa kuwatishia kuwa hayo ni maagizo ya mkurugenzi wa jiji kitu ambacho hakikuwa kweli.

Baada ya mkuu huyo wa soko kuisambaza video hiyo mkurugenzi alilazimika kuitisha kikao haraka ofisini kwake na watumishi wa idara ya biashara na fedha ili kumhoji Ndugu Yusuph Ngenya pamoja na kuwataka wafanye kazi kwa kuzingatia maelelezo, taratibu, sheria na busara badala ya kutaka kufanya kazi kwa minajili ya kuleta taharuki, vurugu na hamaki kwa wananchi wa jiji la Arusha.

Katika kikao hicho mkuu wa soko kuu jiji la Arusha Ndugu Yusuph Ngenya alikiri kufanya kosa la kudanganya kuwa ameagizwa na mkurugenzi wa jiji hilo Dkt Maulid Suleiman Madeni, pili kwa kujirekodi video na kuisambaza jambo ambalo linaichonganisha serikali hususani chama tawala CCM na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli dhidi ya wananchi wa jiji hilo, tatu kwa kukiuka maelekezo ya Mhe Rais Magufuli na mkurugenzi wa jiji hilo. Ambapo aliwaomba msamaha Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli, Mkurugenzi wa jiji hilo Dkt Maulid Suleiman Madeni, wananchi wa jiji la Arusha hususani wafanyabiashara wadogo.

Naye Mkurugenzi wa jiji hilo Dkt Maulid Suleiman Madeni alimsamehe Ndugu Yusuph Ngenya ambapo tofauti na matajio ya wengi waliotegemea mhusika angelala polisi au kusimamishwa kazi mkurugenzi alimtaka aandike barua ili aende akaongeze elimu kwani kwa sasa Yusuph ana diploma ya uhasimu hivyo akasome shahada. Dkt Madeni alisisitiza najua ukiongeza elimu utapata maarifa zaidi yatakayokuwezesha kuitumikia serikali na watanzania kwa ufanisi zaidi.

Pia Dkt Madeni alimueleza Ndugu Yusuph kuwa amemsamehe yeye binafsi na waliomtuma kumkwamisha na kumchonganisha dhidi ya waliomuamini hususani Mhe Rais Magufuli pamoja na wananchi wa jiji la Arusha. Aliwahimiza watumishi wote wanaohusika na ukusanyaji wa mapato watimize wajibu wao kwa kujiamini zaidi na kwa kuzingatia weledi ili kuliingizia jiji hilo mapato mengi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Arusha na kuitekeleza kwa kiwango cha juu ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.

Mwisho aliwatahadharisha kuwa hatamvumilia mtumishi yeyote atakayekubali kutumika na yeyote katika kukwamisha utekelezaji wa ilani ya CCM ndani ya jiji hilo au kuichonganisha serikali hususani Mhe Rais Magufuli na wananchi. Yeyote atakayeingia katika mtego huo ajue hawezi kuwa salama.
IMG_20190301_012310_978.JPG
IMG_20190301_012247_527.JPG
IMG_20190301_012231_086.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao ni wapiga dili mawakala wa mabeberu.

MHUBIRI 4:13 SUV

"Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo."
 
Mwenye shibe hamjui mwenye njaa hivi kwa biashara gani iliyo kuwepo Tanzania kwa Sasa kwa faida gani?
 
Mazingira ya biashara bado si mazuri sana kwa nchi yetu.
Ushuru, tozo, kodi, service levy ni janga kwa sisi wa kipato kidogo.
Ila tunalia machozi kama Mamba ambayo yanamezwa na maji.
No one to help, carelessly!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nimeona hii kitu nikacheka sana ! yaani pamoja na vitisho vyote lakini wakina dada hawakukubali ujinga !
 
Back
Top Bottom