Waheshimiwa nina mgeni ambae sasa Anaelekea kumaliza wiki akiwa hapa kwangu, ni binamu yangu huwa anaishi mkoani amekuja kwa shughuli zake binafsi, ataondoka atapokamilisha yaliyomleta
Nimewaandikia kwa sababu, Huyu jamaa amenishangaza sana, imagine weekend hii iliyokwisha anashinda na boxer kutwa nzima tena kifua wazi, au kwa sababu amevimba kifua anataka tumwone au?
Mke wangu na house girl wanafua nguo jumamosi asubuhi eti anaenda pale awasaidie kufua, Natoka ndani namuuliza wife mbona mgeni anafua nguo, najibiwa kuwa eti ameomba mwenyewe, hii ni sawa kweli?
Yote tisa, kumi ni Jana, inafikia hatua linamkuta wife jikoni anasonga ugali linaomba limsaidie kusonga ugali, mgeni gani wa namna hii?
Wadau nitumie njia gani kulitimua hili jitu hapo nyumbani? Kabla halijaleta madhara maana mdogo wa mke wangu naona kama yuko nalo karibu sana, pia wife kaniuliza kama mm pia naweza kufanya mazoezi nikawa kama hilo jitu badala ya kitambi, Ingawa alinieleza kwa utani huku tukifurahi na kutaniana ila najiuliza kwa nn aseme sasa wakati hili jitu lipo?
Linakaa hapo sebuleni kwenye video hadi usiku mwingi likiwa na mdogo wa mke wangu bila kujali maadili
Jumapili Nilienda kwenye Bonanza la timu yetu ya veterans narudi nimekuta nyumba nzima hawapo wameenda beach wote pamoja na huyu jamaa
Hivi unaendaje ugenini halaf unaanza kuleta ujuaji wa namna hii?
Wadau msaada wa mawazo unatakiwa haraka