Mke wangu ananiibia pesa

Acha pombe
Mwizi ni mwizi tu, hata akiacha pombe atasachiwa tu..

By the way, wizi namna hiyo ni tatizo la kitaifa. Wanawake wengi tu wana tabia hiyo ingawa si wote.

Wapo wanaosachi ukiwa umelala na hujalewa

Wapo wanaosachi ukiwa unaoga au umetoka kidogo
 
Mke anakuibia?...nyie ni mwili mmoja anachofanya mke anatumia pesa iliyobaki baada ya wewe kuitumia mpe pongezi mkeo angekuwa mwingine asingekubari ukatumia pesa peke yako(pombe) angetaka muwe wote
 
Mwizi ni mwizi tu, hata akiacha pombe atasachiwa tu..

By the way, wizi namna hiyo ni tatizo la kitaifa. Wanawake wengi tu wana tabia hiyo ingawa si wote.

Wapo wanaosachi ukiwa umelala na hujalewa

Wapo wanaosachi ukiwa unaoga au umetoka kidogo
ha ha haha aiseee we ni muhanga wa lipi?
 
Mtegeshee wembe ule mkali...kunako hela yako
Ulete mrejesho
 
Haya maelezo yako yameegamia upande mmoja..inawezekana kiasi unachoacha kwa ajili ya matumizi ya familia hakikidhi mahitaji.....na inawezekana mkeo anakuambia na wewe unakuwa kichwa kigumu na kuendekeza starehe ya ulevi.....nina hakika kwa asilimia kubwa mkeo anachukizwa na tabia yako ya ulevi......na ni dhahiri kuwa unapoteza fedha nyingi sana kwenye ulevi na sio kwenye mahitaji ya familia....
Inakupasa kukaa na kuzungumza na mkeo na mkafikia muafa....ni jambo lenye kukera mkeo na wanao wanashindia miharage mpaka wakiyaona wanahisi kizungu zungu alafu wewe unakula kuku kwa mrija huko baa....
 
Sasa kama unakuwa umelewa kiasi cha kutojielewa mkeo anapokusachi, unapataje uhakika kuwa ni yeye anayekuibia. Tumia akili.
 
mkuu nakutegemea hapa mjini muache tu achukue alete nipate za kula na kulipa kodi,ifikie wakat watanzania tuhurumiane,nakuahidi sitompa mimba.
 
Siku moja rudi jifanye umelewa alaf acha hela Humo kwenye wallet au suruali usipoikuta bas anakuibia/ukiikuta ...........
 
Mwizi ni mwizi tu, hata akiacha pombe atasachiwa tu..

By the way, wizi namna hiyo ni tatizo la kitaifa. Wanawake wengi tu wana tabia hiyo ingawa si wote.

Wapo wanaosachi ukiwa umelala na hujalewa

Wapo wanaosachi ukiwa unaoga au umetoka kidogo
Hakuna mke mwizi duniani, anachukua mgao wake kama unabisha mpe mke talaka, ukienda mahakamani mali zako mnagawana 50 kwa 50.
 
kuna braza wangu mke wake naye ni kidokozi hivohivo,

ila anasema, akigundua mkewe amemuibia na kumpa kichapo, mishemishe zinaharibika! akiwa mpole mambo yanasonga balaaa, basi anaombaga kishezi awe anaendelea kudokoa
 
LEWAAAAAAA mpaka aibiwe papuchi nae ndo uje utuulize niache pombe utaombaje ushauri wa kijinga humu mkuu
 
Ndugu wana JF,

Nina mke nimezaa naye mtoto mmoja bahati nzuri Mungu kanijalia kazi ambayo inaniwezesha kupata mahitaji yangu ya kila siku kila mwisho wa mwezi na mpa pesa ya kununua kila kitu.

Cha ndani cha kushangaza kila nikirudi home akigundua nimelewa ananisachi na anachokikuta anachukua nikiamka asubuhi nikimuuliza anakuwa mkali akidai hela yote imeishia kwenye pombe je nichukue hatua gani?
hIYO NI ISHARA YA WEWE KUACHA POMBE NA YEYE ATAACHA KUCHUKUWA CHAKE MAPEMA (soft wizi) !!

STOP DRINKING ALCOHOL... bado mna mlima mrefu kuupanda..tulia ulee mwanao !!
 
Back
Top Bottom