Mke wa Nabii & Mtume Dr H.E GeorDavie anapokuwa First Lady

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
19,931
34,411
Heshima sana wanajamvi,

Leo katika angaika angaika zangu nikajikuta nimeingia Equity Bank Arusha wakati nasubiri kuhudumiwa nikawa natupia macho katika TV ndani ya ukumbi wa Bank.Channel Ten bila chenga walikuwa wakionyesha kipindi cha Nabii & Mtume Mkuu H.E Mstahiki Mheshimiwa Dr GeorDavie akionyesha mbwembwe nyingi wakati bado nashangaa akamwita Mke wake na kumtambulisha kama First lady Mrs GeorDavie ukumbi ukalipuka kwa vigelegele na shangwe kubwa.

Wateja tuliokuwa ndani ya Bank tukabaki kushangaa na kucheka jinsi hawa wanaojiita watumishi wa Mungu wanavyoweza kuteka akili za waumini wasiopenda kutumia akili walau kwa 10%.
 
Unashangaa!! Mbona siku hizi ndio fashion wahubiri wa dini wakitukuzwa sana. Ukiangalia baadhi ya TV utakuta wanazuka kila kukicha. Ajabu ni kwamba katika waumini waokuna watu ambao ni waelewa kama wasomi. Ajabu nyingine manabii hawa wanatajirika haraka sana
 
Sio mfuasi wa Nabii lakini nadhani yuko sahihi, First lady sio mke wa Rais, hili neno lilianzia Magharibi(Marekani) kwenye msiba wa mke wa Rais mstaafu wa Marekani katika kumpamba na sifa za marehemu sikumbuki aliyekuwa akisema ila alitamka "She was the first lady of the land" tangu hapo wake wa marais wakaanza kutambulika kama first lady, lakini nadhani ni sifa ambayo mwanamke wa mtu yeyote anaweza kutumia ingawa kwa sasa ndio hivyo tulishakaririshwa.
 
Ukiwa muumini wa dini yoyote huwezi hoji kila kitu kutoka Kwa mhubiri/shehe wako, hivyo si busara kuwadharau waumini wa mchungaji yule maana huyo ni kiongozi wao na anafanya hivyo km kielelezo cha heshima Kwa mkewe ambaye licha ya yote ni mke wa yy mwenyewe anayejiita na kujulikana km mheshimiwa sana nabii. Let the dead burry their deads!
 
VIP like gari lilipatikana??
Ngongo umenishitua kumbe wewe ni wa ajabu sana,hapo kilichokushangaza kipi???Mbona kawaida tu hata mimi kwangu hivyohivyo tu kwa first lady wangu.wewe inaonekana kwako mko kama paka na panya.
 
Reactions: nao
Mi mke wangu simpendi.sio ndugu yangu wakati wowote anaweza nigeuka.au nifanya chochote
 
Kama
kuna first lady maana yake nabii huyo anaweza kuwa na second lady; nakadhalika! Hivi "first lady" wake huyo ni yule waliyepelekana polisi baada ya nabii "kutusua" kondoo?
 
Hata mimi msichana wangu huwa namuita MALKIA, mtoa mada karibu kwa malalamiko tena ikibidi nenda ukanishitaki kwa yule wa Uingereza.
 
Reactions: nao
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…