Canaan Sodindo Banana (Machi 5, 1936 - 10 Novemba 2003) alikuwa Rais wa kwanza wa Zimbabwe kutoka Aprili 18, 1980 hadi Desemba 31, 1987
Wakati wa uhai wake, Banana ndiye aliyeviunganisha vyama vya hasimu vya siasa nchini zimbabwe, Union Zimbabwe African National (ZANU) na Zimbabwe African people's Union (ZAPU), na alikuwa miongoni mwa wanadiplomasia wa mwanzo kuhimiza kuanzishwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika,
Mwaka 1997 Canaan Banana alishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Mwaka 1998 alifungwa jela baada ya kupatikana na hatia kwa makosa ya kulawiti pamoja na kushiriki vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, mwaka huohuo alifanikiwa kutoroka Zimbabwe kabla ya kusomwa kwa hukumu yake alitorokea South Africa baada ya kukutana na mzee Nelson Mandela, Banana alishawishiwa kurejea Zimbabwe ili akatumikie kifungo chake cha miaka kumi alikubali kurejea Zimbabwe na mnamo tarehe 18 January 1999 aliingizwa gerezani kukabili kifungo ch miaka kumi, ambacho alikitumikia kwa miezi sita tu na baadae mamlaka za zimbabwe zilimwacha huru
Alifariki tarehe 10 mwezi wa kumi na mija 2003 kwa ugonjwa wa kansa huko London uingereza.