Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,106
- 10,173
JamiiForums, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Jukwaa la Katiba (JUKATA), Tanganyika Law Society (TLS), Twaweza East Africa, na Centre for Strategic Litigation (CSL), wametoa maoni kuhusu miswada minne inayohusiana na uchaguzi nchini Tanzania, ambayo imeletwa na Serikali na kusomwa kwa mara ya kwanza tarehe 10 Novemba 2023. Miswada hii inajumuisha Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani; Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Gharama za Uchaguzi; na Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi. Serikali imetoa fursa kwa wadau kutoa maoni kwenye miswada hii kuanzia tarehe 6-10 Januari, 2024.
Katika muswada wa Sheria ya Uchaguzi, wadau wamependekeza mabadiliko yanayolenga kuboresha utaratibu wa uchaguzi na kuhakikisha chaguzi ni huru, za haki, na za uadilifu. Wamesisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika utambuzi wa wapiga kura na uwepo wa midahalo kwa ngazi zote za uchaguzi.
Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa wamependekeza mabadiliko muhimu kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019. Kwa kuwa baadhi ya vifungu vinahitaji marekebisho ili kuhakikisha vyama vya siasa vinazingatia katiba na sheria nyingine za nchi.
Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi unalenga kuongeza uwazi na uwajibikaji katika masuala ya fedha katika uchaguzi. Hili ni jambo zuri katika kujenga demokrasia yenye uwazi na uwajibikaji kwa wadau wote.
Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wamependekeza kuanzishwa kwa sheria inayojitegemea kuhusu Tume ya Uchaguzi. Wamependekeza maboresho katika muundo wa Tume ili kuifanya iwe huru na isiyoingiliwa na mamlaka nyingine katika majukumu yake.