Jana nilisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea Singida. Nikaona nitumie usafiri wa Treni mpaka Dodoma asubuhi kisha niunganishe bus kutoka Dodoma kuelekea Singida.
Nilifanikiwa kufika mapema Dodoma kwa treni. Dhahama ikaanzia nilipofika kituoni kutafuta usafiri wa kwenda kituo cha mabasi cha nanenane ambacho kipo umbali wa km 8 kutoka kituo cha treni maarufu sgr.
Swali lilipita kichwani lilikua hivi kuna mawasiliano ya mipango miji wakati wa ujenzi wa vituo hivi. Kwanini havikuwekwa karibu na kama si pamoja. Muda, usumbufu na fedha inayotumika kwa msafiri ingefanya mambo mengine ya msingi.
Je kuna wakati watakuja wataalam waseme walikosea kisha waweke city train ili kuunganisha stendi ya bus na sgr? Wabomolee watu na kulipa fidia.?
Ni vyema tujitafakari kama nchi na utaalam wa wanaofanya kazi za usanifu miji, mipango miji na watoa maamuzi ili tusije kutukanwa na vizazi vijavyo.
Ili la umbali wa kituo cha sgr Dodoma na nanenane stand liangaliwe na kufanyiwa kazi.