Mimi hupendelea kuhifadhi sarafu, roho yangu inaridhika kuziona na pia huwa zinavutana

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,286
50,380
nilianza kuzipenda sarafu kipindi nauza duka nilikuwa naziweka kwenye bag zinakaa muda mrefu kwa kuwa maduka ya jumla hawapendi kupoteza muda kuhesabu chenji chenji.

Siku hizi siuzi tena duka niko na mishe nyingine na Nimekuwa na changamoto ya matumizi mabaya ya pesa yaan unapewa leo million moja baada ya siku 5 yote umeitia chini ya pua unaanza kulia lia kuomba omba.ninachokifanya sasa kama solution ni pale napopewa pesa naenda bank na katika masoko naanza kuchenji nipewe sarafu za 200,500,100 kama ni laki tano nakuwa na bonge la mzigo wa masilesile, yale yanakaa hara miezi 3 kwa kuwa utaji tune kutumia matumizi madogomadogo hutashawishika kwenda club na li mzigo la machenji ya 50000.

Kingine sasa huwa najisikia raha najiona tajiri kwa kuwa kila hela nayopata natamani nikaombe chenji ili nikayatupie na masarafu menzake..kwa ufupi sarafu zinavutana zenyewe zinatabia ya kujaa.

Kwa sasa nina mpango wa kuchimba shimo chumbani kwangu ili niwe nayafukia kwenye kibubu cha chuma nayaficha, sitaki tena makato ya simu wala biashara ya kuweka bank.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…