Milipuko yatokea uwanja wa ndege Brussels, 34 wapoteza maisha

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Milipuko miwili imesikika kutoka uwanja wa ndege wa Brussels ambapo watu wanaondolewa. Shuhuda anasema alikuwa katika eneo la uwanja wa ndege wa Zaventem na kusikia milipuko miwili yenye sauti kubwa sana.

"Niliweza kuhisi jengo linahama, kulikuwa na vumbi na moshi pia. Nillielekea mlipuko ulikotokea na kulikuwa na watu wanatoka nje huku wamekumbwa na kiwewe na mshtuko".

"Fikra zilizoko hapa ni shambulio la kigaidi ambalo bado halijathibitisha na mamlaka yoyote kwenye uwanja."

Watu wasiopungua kumi wanahofiwa kufa kwenye shambulio hilo.


Muendelezo: Idadi ya waliofariki kwenye tukio hilo imefika watu 34


========

Two loud explosions have been heard at a Brussels airport which is being evacuated.

Sky's Alex Rossi, at the scene, said: "I was in the duty free in Zaventem Airport and I heard two very, very loud explosions.

"I could feel the building move. There was also dust and smoke as well.

"I went towards where the explosion came from and there were people coming out looking very dazed and shocked."

"The thinking here is that it is some kind of terrorist attack - that hasn't been verified by any of the authorities here at the airport."


Source: Sky News
============

UPDATE

Several dead and wounded at Brussels Airport, Belgian federal police confirm to NBC News.
============

UPDATE

Ten Dead In Brussels Metro Station Blast

At least 10 dead have reportedly been killed in a rush-hour explosion at a metro station close to EU Buildings in Brussels.

Footage of the blast at Maalbeek station showed black smoke pouring from the entrance.

Passengers were evacuated from trains in the tunnels around Maalbeek.

Outside the station, people were being moved on stretchers and others were seen with facial injuries.
============
UPDATE

Ndugu waliojilipua Brussels watambuliwa


Washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga waliojilipua katika uwanja wa ndege wa Brussels Jumanne wametambuliwa kuwa ndugu wawili, Khalid na Brahim el-Bakraoui.

Kituo cha runinga cha RTBF kimesema wawili hao walifahamika vyema na polisi.

Mwanamume wa tatu aliyeonekana kwenye video za kamera za siri uwanja wa ndege akiwa pamoja na wawili hao bado anasakwa.

Milipuko miwili ilitokea katika uwanja wa ndege na mwingine mmoja katika kituo cha treni na kuua watu 34 na kujeruhi wengine 250.

Ubelgiji imeanza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

RTBF imesema ndugu hao wawili walifahamika na polisi na wana rekodi za uhalifu lakini hawakudhaniwa kuwa na uhusiano na ugaidi awali.

Kituo hicho cha runinga kimesema Khalid el-Bakraoui alitumia jina bandia kukodi nyumba katika eneo la Forest jijini Brussels ambapo polisi walimuua mtu mwenye silaha kwenye makabiliano wiki iliyopita.

Ilikuwa ni wakati wa msako huo ambapo polisi walipata alama za vidole za Salah Abdeslam, mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris ya 13 Novemba.

Abdesalam alikamatwa kwenye operesheni ya maafisa wa usalama Ijumaa.
 

Attachments

  • CeIqpUlUIAAUbhf.jpg
    17.2 KB · Views: 82
  • CeIryJpUsAAJOGB.jpg
    18.9 KB · Views: 81
  • 160323105527_suspect_brussels_512x288_bbc_nocredit.jpg
    20.7 KB · Views: 70
Yaani mimi ningekuwa raisi wa moja ya nchi za ulaya,nisingepokea hata mkimbizi mmoja kutoka syria kila siku wanakimbilia ulaya,huko baadae watoto wao watakuja kuwa magaidi ,yaani hawa ulaya yaani wangestop kabisa kuwapokea hawa refugees
 
Inasikitisha sana...Marekani hafai ktk huu ulimwengu jamani...vikundi vyake vinafanya kazi yakuuwa watu wasiokuwa na hatia, syria hivyo hivyo Nigeria nako hivyo hivyo, kenya pia..kazi kweli kweli
Mkuu

Swala la wakimbizi wa Syria huko Europe ni mpango wa Russians.

Mwanzoni Russia alikuwa soft sana juu ya Europe kwa sababu aliamini kuwa Europe ni ndugu yake. Tatizo la Russia lilikuwa juu ya US tu.

Sasa, NATO alivyoanza encroachment towards Russians pamoja na vile vikwazo batili, hapo Russia ikaona "huyu anatuchezea".

Alichokifanya Russia ni ku pump more refugees to Europe. Europe kuja kustuka ni too late.

Na huu ni mwanzo tu bado ngoma ni mbichi kabisa. Mpaka Europe wasambaratike. Kwa sababu mwisho Wa Siku hizi nchi zitatofautiana kuhusu hawa wakimbizi.

Pia leo hii Military Commander wa Russia amesema wataanza tena mashambulizi kwa wale waasi wanaovunja makubaliano ya ceasefire.
 
Hawa ISIS wanawajuaje wayahudi,maana jana uturuki,waisrael wamekua targeted,leo pia sehemu mbili tofauti target ni haohao,
safari za ndege kutoka ulaya kwenda israel zimesimamishwa kupisha uchunguzi
 
Mlipuko mkubwa umetoka katika uwanja wa ndege wa Brussel Ubelgiji. Kutokea kwa mlipokuo huo kumesababisha safari za ndege kukatishwa na watu wote kutakiwa kutoka uwanjani hapo. Mlipuko huo umetokea siku nne tu baada ya mshukiwa mkuu wa shambulio la Paris (Ufaransa) Salah Abdeslam lililofanyika tarehe 13 Nov 2015 kukamatwa akiwa Brussels Ubelgiji. Mpaka sasa watu haijafahamika idadi kamili ya watu waliofariki au kujeruhiwa.
 
Inasikitisha sana...Marekani hafai ktk huu ulimwengu jamani...vikundi vyake vinafanya kazi yakuuwa watu wasiokuwa na hatia, syria hivyo hivyo Nigeria nako hivyo hivyo, kenya pia..kazi kweli kweli
inaonekana mbwa kaamua kumuuma mwenye mbwa sasa,
very very bad,
 
Yaani mimi ningekuwa raisi wa moja ya nchi za ulaya,nisingepokea hata mkimbizi mmoja kutoka syria kila siku wanakimbilia ulaya,huko baadae watoto wao watakuja kuwa magaidi ,yaani hawa ulaya yaani wangestop kabisa kuwapokea hawa refugees
Ni hao hao wazungu kwa sera kandamizi dhidi ya magaidi ndiyo zinazozaa ugadi na wamezichonganish nchi zao sasa wameamua kuwafuata kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…