Mustaphagentleman
JF-Expert Member
- Jun 22, 2016
- 3,953
- 3,020
Shamba la Bibi vuna unavoweza
Kha.!Wageni wanakuja kufwata nini wakati muda wa kututawala ulishafika kikomo tena natamani hawa watu wasije kabisa kwani utalii ni nini bwana wakae kwao wauze mahindi sio kuja kutusumbua k koo na mitaani
Hatuwezi kubadilisha maisha yetu kwa ajili ya mgeni, ningeelewa kama hoja ingekuwa kwamba Watanzania tunapata tabu Airport lkn siyo mgeni!
Kodi si ndiyo inakusanywa lakini jamaa yako anakuna na mada za kusema wanaonewa?Ndio zamani nilisema, 'upumbavu ni mzigo' na 'akili nzuri ukiwa nayo'.
Yaani wewe unafikiri uchumi wa nchi utaendeshwa na kodi zinazotokana na mifuko ya wananchi, bila kujua kuwa baadhi ya hao wananchi wameajiriwa na International Organizations ambazo zinahitaji mazingira bora ili ziendelee kuwekeza.
Sikiliza nikuambie: huo uchumi mnaosimuliana Lumumba, hauletwi na majipu wala maagizo ya kila uchao ya kukamata wasio na kazi na shisha. Kuna watu wanaingia JNIA na ndege ya KQ ya saa 2 asubuhi, wahudhurie meeting Kempinski saa 8 wawe tena airport kwa ajili ya kurudi Nairobi kwa meeting nyingine. Kama haya we huyajui, unafikiri kwa akili ndogo ndogo tu ya kushindana na ombaomba.
Watalii hawaji kwa basi za mwendokasi, wanakuja na ndege na wanafikia hapo unapopazungumzia kama unaongelea kilabu cha pombe za kienyeji. Baadhi ya mambo waachieni watu wenye akili timamu wajibu, sio kila kitu kijibiwe na kamati ya siasa jamani.
Hapo hiyo siyo hoja yangu. Mimi nimemjibu anayesema hakuna haja ya kuboresha kwa kuwa wageni hatuna haja nao, kama upo kwenye hilo jibu kwenye hilo. By the way, muanzisha mada hajasema wasilipe...kahoji risiti ina maana ana mashaka na udhibiti wa mapato, au wewe umemuelewaje?Kodi si ndiyo inakusanywa lakini jamaa yako anakuna na mada za kusema wanaonewa?
Ukitaka VISA ya America, unapewa akaunti namba unakwenda mwenyewe kulipia Citi Bank. Swali lingine?Hivi ukienda ubalozi wa marekani , uk, n.k kuomba visa unapewa risiti?
Mbona unaongea kama haujaenda shule kabisa. Yani unadiriki kusema wasije kabisa, au unaelewa nini unaposikia wageni. Tena tunakamsemo ketu: "mgeni njoo mwenyeji apone". Mtoa mada na nia njema ya hela ya umma isipotee halafu wewe unaleta maruhani yako, kisa bando unalo.Wageni wanakuja kufwata nini wakati muda wa kututawala ulishafika kikomo tena natamani hawa watu wasije kabisa kwani utalii ni nini bwana wakae kwao wauze mahindi sio kuja kutusumbua k koo na mitaani
Wanakudharau wakiwa na sababu....na moja wapo ni ujinga kama huo hapo airport. JIREKEBISHE ndio dawaWacha wageni waisome namba tukienda kwao wanatubagua sana nakushangaa mtoa mada kuwatetea mabeberu kimsingi sitaki hata kuwaona hapa bongo maana wanatuzarau sana
Hatuhitaji Raisi hapo hata Katibu mkuu wa wizara anatosha kumaliza huu ujingaViongozi wa uwanja wandege na maofisa wa uhamiaji ni majipu ambayo Mheshimiwa Rais Magufuli itabaidi ayatumbuwe ni aibu kubwa wanapo kuja Wageni.
Mkuu hongera kwa thread yako. Naomba uongeze na hii ya kuomba visa online kama wanavyofanya kenya. Mgeni anafanya application online, analipia online na kupelekewa visa yake kwa email. Anachofanya ni ku-print na kuanza safari. Kenya Visa Online, Express Kenya e Visa.Mheshimiwa Rais, labda hili litakuwa gumu kidogo kwa wewe kuligundua maana viongozi wote wanapopita pale uwanjani huwa hawatumii njia na process hii ambayo sisi watu wa kawaida na wageni wanaotoka nje huwa wanaitumia katika kupata viza (tourist visa) ya kuingia nchini.
Pale kuna uozo mkubwa sana na si hilo tu basi upoteaji mkubwa wa fedha za serikali ambazo nadhani huwa zinaingia mifukoni mwa baadhi ya wafanyakazi na viongozi wao, ni mtandao ambao upo kwa muda mrefu tu. Ni usumbufu kwelikweli usiokuwa na sababu yoyote.
Sasa ninaelezea kwa kirefu:
Wageni wengi wanaokuja Tanzania na kuchukulia visa zao pale aiport huwa wanatozwa dola za kimarekani 50 ($50.00 Usd) na huwa hawakubali aina nyingine yoyote ya pesa isipokuwa dola za kimarekani tu. (hilo ni tatizo namba 1).
Wageni wanapofika basi kuna mtu (sijui ni nani na anatoka department gani) husimama pale na kukusanya passport zote na hizo dola 50 (kila passport huwekwa dola 50 ndani yake) huyo mtu huzikusanya bila hata ya kutoa risiti yoyote,(na kuwaambia msubiri) na kuenda nazo kusikojulikana (labda ni ofisini kwao) kwa ajili ya kuweka hizo viza, hapo sasa ndiyo kuna tatizo kubwa sana, Mtasubiri si chini ya saa moja ndipo mtarudishiwa passport zenu na viza tayari zimo ndani, akifika huyu mtu anaanza kuita majina na kukukabidhi passport zenu ili sasa muelekee uhamiaji kwa ajili ya kupata entry ya kuingia, wakati huo sasa wale wenzenu wote mliokuja nao wameshamaliza kupita kwa watu wa forodha na wako nje tayari.
Nimesikia kwa sasa hivi huyo mtu wa kukusanya hizo passport hayupo ila walichofanya ni kuweka kijiofisi kidogo ambacho hufanya hivyo hivyo, unafika pale kwenye hicho kijiofisi na kumpa passport na dola 50 (hawataki aina nyingine yoyote ya fedha) na HUPEWI risiti yoyote, halafu unaambiwa usubiri, baadaye anakuja mtu kuzikusanya passport zote hizo anaenda nazo ndani huko, hapo bado tena mtasubiri siyo chini ya saa moja au mawili ndiyo mrudishiwe hizo passport. Mimi nilishuhudia wageni wenye asili ya kizungu wakilalamika sana pale airport kuhusu huo usumbufu.
Sasa mimi maswali yangu ni kwa nini wanapenda kuwafanyia watu huu usumbufu? na hapo ni dhahiri kuwa kuna pesa nyingi tu ambayo badala ya kwenda serikalini basi huingia mifukono mwa watu.
Sasa Mheshimiwa Rais kama tuko kwenye kuitengeneza Tanzania hii kuwa nzuri, bora na ya uwajibikaji, kwa nini basi usisafishe na kulitatua tatizo hili? Mimi naamini kabisa kuwa wageni wengi wanaokuja TZ wakishapata usumbufu huu basi huwa hawarudi tena na badala yake wanakwenda nchi jirani.
Nini cha kufanya:
Nimetembelea nchi nyingi ambazo hutoa viza palepale airport na hukuti matatizo kama haya kwa sababu hakuna wizi.
Nchi 1: Hapa ukifika tu utakuta kuna ofisi, unaenda dirishani unampa passport yako na pesa au bank card (pesa ya kigeni yoyote inayotambulika, zote zimeorodheshwa pale), palepale anakubandikia visa (sticker) na unaelekea kwa uhamiaji. Kitendo hicho hakichukui hata dakika 5.
Nchi 2: Hawa hawataki fedha taslimu kabisa, ni bank card tu, ukifika tu unaenda kwa uhamiaji moja kwa moja, pale unafanya malipo kwa bank card yako, unapata risiti na anakugongea viza (mtu huyohuyo mmoja), kwa hiyo yeye hakamati fedha taslimu kabisa. Hapa sasa tunaweza kusema kwa wale wasio na card je? Jibu ni hivi, kwanza watu wengi wanaoomba viza hapo airport ni wageni na ndiyo maana wanaomba hizo viza, kwa asilimia kubwa ya hao watu wanazo kadi, na pili unaweza kununua Prepaid visa/mastercard, kwa wale wanaoishi ughaibuni watanielewa, kupata bank card huko ughaibunu siyo big issue.
Nchi 3: Hawa sasa ukifika unaenda dirishani kulipa kwa bank card au fedha taslimu, halafu anakupa risiti unaenda nayo kwa uhamiaji na passport yako na uhamiaji anakupigia entry visa kwenye passport yako na kwenye ile risiti, hapo huchukui hata dakika kumi.
Sasa mimi sisemi tuige hayo hapo juu (lakini kama ni mazuri kwa nini tusiige?) lakini tukichukua yote hayo na kuyachanganua vizuri basi tunaweza kutengeneza mfumo wetu wenyewe ambao hautampa mgeni usumbufu hapo airport. Pili ningependa pia kuiomba serikali hizi balozi zake ziwe zinajaribu kutoa visa kwa waombaji wake kwa haraka kidogo ili kuondoa nenda rudi nyingi.
Mimi naamani kabisa kuwa hilo tatizo linaweza kutatulika na mtiririko wa wageni unaweza kuongezeka, maana wenzetu wageni huwa hawapendi usumbufu, kwanza huwa wanakuja kutembea na hivyo huwa hawapendi kupata bugudha kama hizo hasa ukizingatia kuwa Airport ndiyo kioo cha nchi, maana ya kwamba mgeni akiona mwenendo wa pale airport (airport yoyote duniani) basi tayari inampa taswira ya nchi hiyo ilivyo.
Kwa hiyo Naomba Mheshimiwa Rais na waziri husika mlifumbulie macho suala hili, Fedha za serikali pale airport bado zinaliwa na wajanja.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki JPM
Kufwata!!! Hiki kiswahili cha Watz wenzangu, yaani ni majanga tu. labda nikujibu kwa kukuuliza swali. Waafrika nao wanaenda ulaya na Marekani kutafuta nini wakati muda wa kutawaliwa ulikwisha? Ni nani aliyekwambia kuwa nchi zilizoendelea zinategemea kuuza mahindi ndio waishi? halafu ni vema ukajua kwamba katika Dunia hii huwezi kuimarika kiuchumi kwa kujitenga na kuzuia wageni kukanyaga kwenye nchi yako.Wageni wanakuja kufwata nini wakati muda wa kututawala ulishafika kikomo tena natamani hawa watu wasije kabisa kwani utalii ni nini bwana wakae kwao wauze mahindi sio kuja kutusumbua k koo na mitaani
Wewe mleta mada ni miongoni mwa vigeugeu wakubwa humu jf. Huwa unapenda sana kuna mada zako zinazoelezea namna serikali inavyotukuza wageni na kuwapuuza wazawa, leo unawatetea. Ukinyonga mtupu