Ni maoni yangu tu, mheshimiwa hii wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano kiukweli ni kubwa mnoo.
Nakumbuka hii ya ujenzi ulikua wewe na ulikua unaona ulivyokua unazidiwa na safari kwenda kukagua miradi, na ndy maana makandalasi walikua wanajitahidi, ila kwa sasa mh mbalawa hatoweza.
Hii itapelekea miradi mingi utakayo ianzisha haitakua na ubora ule unao takiwa, kama unavyo jua hasa Tanroads ndy kuna watu wenye uwezo wa kupiga bila mtu yeyote kujua na ndy sehemu ambayo ikisimamiwa vizuri taswira ya nchi inabadirika.
Pia utambue kwamba mtu anapokua waziri si muda wote anafanya mambo ya kiuwaziri anahitaji muda pia afanye mambo binafsi ya kijamii.
Mapendekezo yangu; Huyu waziri wa sasa abakie ktk uchukuzi na mawasiliano. Pia tafuta senior Engineer kutoka ktk kampuni kubwa ndy umpe uwaziri wa ujenzi.
Ahsante naomba kuwasilisha.