Mh. Msigwa umeonesha ukomavu katika siasa

Mzalendo39

JF-Expert Member
Apr 17, 2015
881
1,033


Ni katika viwanja vya Karimjee leo wakati bunge likimkabidhi Mh. Rais madawati kwa ajili ya watanzania

Mh. Mbunge wa Iringa alionekana akiwa kwenye ratiba hiyo na hata kupiga picha na Mh. Rais pamoja na wabunge wengine.

Kinachonishangaza ni vijana wa CCM na CHADEMA wanapomponda na kubeza kitendo hicho ambacho kinaonekana kwenda tofauti na msimamo wa chama chake, baada ya CHADEMA kutangaza msimamo wake kwa kutoshirikiana na serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Msimamo huo ulianza wakati wa vikao vya bunge la bajeti vikiendelea Dodoma pale walipoonyesha msimamo wao wa kutoshirikiana na naibu spika na kuanza kususia vikao vya bunge ambapo ilifika mbali hata kisusia wabunge wa CCM na hata kupeana salamu na katika mwezi mtukufu wa ramadhani walisusia futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu pamoja na spika wa bunge

My take:
Huu ni wakati wa kuwa wamoja katika shughuli za maendeleo kwa watanzania.....tofauti za kichama zisituwawe watanzania


Naungana na Mh. Msigwa pamoja na watu wote wanaounga mkono utaifa kwanza vyama baadae.
 
There is a thin line between ukomavu and unafiki, Msigwa has just manifest the later.
 
Hivi walitangaza kususia shughuli za serikali au vikao vya bunge vinavyoongozwa na NS Dr Tulia Ackson?

Mimi naona kama umepotosha hapo, sivyo ninavyoelewa mimi, unless niwe nimesahau.....basi nikumbushe..

UVCCM mitandaoni wasikupotezee muda
 
Msigwa kashiriki shughli aliyokuwepo Tulia, kweli usipokuwa na msimamo unaweza kuonekana kituko.
Tukio lile kiongozi hakuwa Tulia, Nate kaalikwa tu kama Msigwa msiootoshe maana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…