Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
MFALME WETU ROPOKIZI.
Eeh Mfalme Juwa,
Mfalme wetu wa ajabu, watawala huongozi,
Sote twapata adhabu, mashavu tele matozi,
Umetutia ububu, kuamba hatukuwezi.
Eeh Mfalme Enze enze,
Hivi sasa aghalabu, kufungwa kwa uchochezi,
Mahakama zetu tabu, zapangiwa maamuzi,
Haikupona maktabu, nayo yatia jelezi.
Eeh Mfalme Jeuri,
Bunge lakula kababu, zilizoungwa na rozi,
Mpishi ni weye babu, mwenye fikira tatizi,
Hii ndio asbabu, kupitishwa upuuzi.
Eeh Mfalme Ropokizi,
Watisha kwa lako gubu, kutwa domo liko wazi,
Waropoka kwa ghadhabu, mfiwa hubembelezi,
Hakika huna adabu, wewe bwana ropokizi.
Eeh Mfalme Katili,
Muda wenda taratibu, ka jua halichomozi,
Ela twafanya hesabu, saa siku na miezi,
Yaja siku ya dhahabu, jua utasema mwezi.
Eeh Mfalme Rahimu,
Mwisho nafunga kitabu, huu sio uchochezi,
Mesema yanotusibu, na kututoa machozi,
Ewe bwana tahdabu, koma wako ubazazi.
19 January 2017.
Shairi langu lingine bofya linki hiyo chini.
Ana mazonge mfalme
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whats app 0622845394 Morogoro