Meno ya mwisho AKA magego

Pelly

Senior Member
Mar 26, 2013
165
164
Habari zenu wana JF?
Naombeni msaada wenu kwa anayejua wapi nawezapata daktari au hospital ama nifanye nini, nimekuwa na shida ya meno au dental formular yangu si nzuri, nimekuwa nikisumbuka na magego ya juu hasa kwa upande wa kushoto mpangilio wake umetengeneza uwazi na jino lingine hadi ninapokula chakula kinaingia kwenye huo uwazi halafu inatengeneza harufu na kuoza.

Kuna watu wamenishauri nikaling'oe lakini nasikia meno ya juu especial magego kuna mishipa inaenda hadi kwa ubongo so ukilingoa tu unaweza kusababisha ugonjwa wa afya ya akili, je mnanishauri au mnanisaidiaje ndugu zangu.

Natanguliza shukurani
 
Back
Top Bottom