Membe: Magufuli anawafukuza watumishi kiurahisi kwakuwa hakuwateua yeye

Hivi kwani Magufuli anaweza kumfanya nini Membe?



Kama Raisi wa JMTZ akiamua anaweza kufanya maisha ya Membe yakawa magumu ndani ya TanZania ana huwo uwezo ni swala la kama Raisi Magufuli ni mtu wa namna hiyo yaani visasi, sifa ambayo Raisi Magufuli hana yeye ni mtu wa Dini na mchapakazi anachofanya Raisi Magufuli ni kuchapa kazi na sasa ripple effect yaani yale mawimbi yanawafikia wazembe na wezi na bado wengi watalia hasa kwenye Mambo ya Gesi na Madini nina uhakika Raisi Magufuli ameshaipitia mikataba yote na tayari ameshaamua cha kufanya rejea kuahirishwa kwa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, swala la UDA ambapo wenye mabasi hawajalipa kodi zetu na mradi mpaka leo hii haujaanza na Mkuu wa DART alishafukuzwa/kusimamishwa na mpaka kushughulikiwa kwa wezi wa Tanzanite yetu!

Na sasa huko kwenye Mafuta na Tanesco ni balaa tupu na Raisi Magufuli anapitia kote huko ndiyo maana alijifungia Ikulu alikuwa anapitia madudu yote, na soon vilio vitaanza kila kona!

Lakini uzuri wa Katiba yetu nim kwamba hakuna kitu watamfanya Raisi wa JMTZ sana sana wao ndiyo watapoteza kama wakiamua kulianzisha!
 
Sasa labda tumuulize ye membe alikuwa anatakaje? Mbona mkwere kateua serikali ya kishkaji mpaka siku anaondoka ikulu? Huyu membe hataki magufuli nae aunde serikali yake? Huyu membe atakua anavuta bangi ya Malawi siyo bure
Kama hiyo uliyovuta.
 
Mheshimiwa mstaafu
Mimi ninacho jiuliza je Membe kajipima na kujiona
'anam mudu Magufuli'?

manake wengi wanatamani kumkosoa Magufuli hadharani lakini ujasiri tu hawana
wanabakia kusema 'Rais anafanya kazi vizuri tumuunge mkono'
Mheshimiwa mstaafu hebu kaa utathmini nchi yetu wote haina haja kucheza na media nakuonyesha gap lako na Mh Rais kwan ana mission na vision zake kuipeleka nchi mbele kwa kubana majizi na mafisadi
 
Membe tangu lini akawa mkosoaji wa viongozi wa serikali ya ccm? Kuna kitu hapa...(time will tell).
 
Membe anataka kutengeneza issue na JPM ili akitumbuliwa aseme ni kwa sababu alimsema Rais. Ukweli unajulikana jipu lake linakaribia kutumbuliwa kwani kuna madudu mengi alivyokuwa waziri wa mambo ya nnje.
 
Hii movie inaelekea pazuri soon tutajua Mengi. Lowassa ubarikiwe kwa kuja Upinzani na kukatwa
 
Naogopa kukubaliana na mitazamo yako, ningependa utambue kuzungumza uongo japo kidoogooo ni dhambi.
 
wanaomsifia magufuli kwa kila kitu wanampotosha njia kwangu mimi amefanya makosa makuu 6 tangu aingie madarakani
Nadhani tuende na hoja kwa hoja. Membe anaposema Rais Magufuli anawafuta kazi watumishi kwa sababu hakuwateua yeye na wala hawaju. Napata ujumbe kuwa kama mtumishi unamjua, hata kama ana makosa ya kiutendaji hupaswi kumgusa kwa sababu za ujuani. Uteuzi wa JK ulizingatia ujuani na siyo utendaji. Wanoafutwa kazi hawana makosa yoyote isipokuwa Magufuli anawatoa tu ili awaweke anaowajua na akiwaweka anaowajua hatawachukulia hatua hata kama wana makosa. Wote ambao Rais Magufuli hajawachukulia hatua walioteuliwa na serikali iliyopita anawajua, amewafukuza kazi wale tu asiowajua.
Hata kama kukosoana kupo lakini kwa hoja kama hizi ni upuuzi hakuna faida ya kukosoa. Membe anaweza kuthibitisha hoja yake hii kwa utafiti gani alioufanya lini na wapi. Kumbe mtu anaweza kuwa kachero na kushika nafasi nyingi na nyeti, lakini asiweze hata kujenga hoja zenye mshiko. Anathibitisha kuwa alipewa nafasi zote alizopewa kwa sababu kulikuwa na mtu anayemjua na mtu huyo hakumfukuza hata pale alipofanya makosa kwa sababu tu za ujuani siyo kwa utumishi uliotukuka
 
Membe yuko sahihi na nilisema toka mwanza kufukuza siyo vibaya lakn uzingatie dheria na kanuni.
 

Mkuu heshma kwako..

Nikiku kunukuu *Membe ni Jasusi Mkongwe hawezi kufanya kosa la kizembe namna hii tena anapangwa Bashe kumjibu sio Kiongozi yoyote ndan ya Chama. Maoni mazito kama hayo hayakutolewa kwny Press conference badala yake kimetafutwa chombo kimoja tu kuzungumze nae.*

Hili jambo uliloweka hapa ndilo Linalozua maswali mengi kua nyuma yapazia kuna nini hasa.
Tuvute subira muda utatupa majibu..
 
tukii pata watu kama akina membe 1000 tutaendeleaa ..in life we need challenges kumbuka bila challenge hata magufuli asingekuwa raisiii.. namsapoti membe kwa sababu atamfanya magufuli asijisahau kama yule naniiiii alotoka juz ikul...........
Hatujatai kukosoa, lakini tunaona hakuna logic ktk vitu anavyokosoa; ok, anasema rais anawafukuzuza watumishi kirahisi, je anataka kutuambia kwamba watumishi wasiotimiza wajibu na wanaohujumu taifa waachwe tu eti kwa sababu hakuwateua yeye? Anasema rais asiwabane Sana wafanyabiashara, je kama wanakwepa kodi waachwe tu? Anasema kuthibiti safari za watumishi wa umma kwenda nje ni vibaya, je anajua kuwa ma-CEO walikuwa wanahujumu taifa kwa safari za nje zisizo na tija nakushinndwa kukaa ofisini kuwahudumia wananchi? Ukiamua kukosoa, basi walau uwe na logic na ba utoe altenatives.
 
Anayoyasema membe leo na kuonekana hafai yatakuja kuonekana baadae ila kwa sasa anaonekana mpuuzi .hata mzee six alisema anashauriwa vibaya
 
This is more of a personal squabble than statesmanship. Mbona mambo mengi yalikuwa yanaenda kombo wakati wa Kikwete na yeye hakuthubutu hata mara moja kuongea au kukemea? Je huu si wivu kwamba mtu ambaye hakutarajiwa wala kutajwa na wengi (JPM) kawa rais wakati yeye na mpinzani mwenzake Lowassa wako pembeni wanachoma Mahindi? Mbona Lowassa mwenye kura milioni 6 ametulia, yeye aliyekatwa na kuzidiwa hata na January Makamba anatuuzia maneno?

WanaCCM muungeni mkono rais ambaye mmemteua kama chama, sisi wengine tulikuwa na chaguo letu lakini baada ya uchaguzi tunashirikiana na rais na tunasonga mbele. Heri basi ya Sophia Simba na Nchimbi ambao walipinga mchakato wazi wazi maana tunajua wako upande gani. Membe, ndo maana tulikukataa, wewe ni kibajaji wa JK. JK akisema nenda kulia au nenda kushoto unaenda. Hata sasa umetumwa, sio bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…