Media inafaidika nini kudanganya Umma? Waliokufa ajali ya Matumbi ni zaidi wengi ajabu.

Watanzania ni watu wa ajabu sana, unajua nani anatakiwa kuthibitisha kifo? Unaweza kutofautisha mtu aliyezimia na aliyekufa kwenye ajali kwa kuangalia kwa macho? Na wale majeruhi waliotangazwa walienda kuokotwa kwenye ajali yingine? Sio kila ajali mnayoiona mbaya inaondoka na watu wengi. Fikiria kama umepita shule kidogo.
 
Mmoja wa majeruhi ni jamaa yangu. Si kweli kwamba walikufa watu wengi kuliko idadi inayotangazwa. Taarifa zinazotolewa ni sahihi. Sijui mleta uzi unamaslahi gani na hili.
Mmoja wa majeruhi ni jamaa yangu. Si kweli kwamba walikufa watu wengi kuliko idadi inayotangazwa. Taarifa zinazotolewa ni sahihi. Sijui mleta uzi unamaslahi gani na hili.
Wewe ni mmoja Wa Wachawi waliosababisha hiyo ajali pumbavu weye.
Haiwezekani unachoongea hakieleweki, eti idadi idadi iliyotangazwa ni sahihi, Kwa hiyo watu wawili ndo wamefariki?

Acha tabia za kichawi we...
 
Bangi bana!!

Kwa nini unasema bangi? hiyo siyo taarifa katika ajali hiyo? Baada ya kuzungumzia taarifa za watu katika ajali hiyo, ilipaswa hilo nalo lisemwe watu wajue idadi ya ng'ombe waliokufa kwenye ajali hiyo na jumla ya ng'ombe waliokua katika gari. Hiyo nayo ni habari mkuu, kwa sababu imetokea katika tukio moja.
 
Taarifa iliyotolewa na Mganga mkuu wa hospitali inasema ni watu wanne wanaume watatu nafikiri na Mwanamke mmoja, hayo mengine ni uzushi, majeruhi 25
 
Umri wangu sio kama wa akina Mzee Kingu lakini pia sio wa akina Milald Ayo, kwa maana kwamba nimeshuhudia baadhi ya matukio mabaya na mazuri katika nchi hii na nje ya nchi. Hili pia kwangu ni tukio la kusikitisha sana na hasa kwenye swala la uzembe wa binadamu na kama kuna ufichaji wa habari wowote ni wazi tutaendelea 'kumsingizia' Mungu badala ya sisi wenyewe kujirekebisha.
Lakini kikubwa kabisa katika hili ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona taarifa ya ajari juu ya majeruihi na wahanga ikitolewa kwa staili hii! R.I.P wote waliohusika na poleni kwa wafiwa.
IMG-20160309-WA0010.jpg
.
 
Kama hali yenyewe ndio hii basi JF iondowe ile kesi yake mahakama kuu kupinga sheria ya mtandao, maana mpuuzi kama huyu mleta mada vyombo vya dola vikimuhitaji mnapaswa mumkabidhi ashughulikiwe ajuwe madhara ya uzushi.

Je yeye anakunywa damu za watu kwamba hajatosheka na idadi ya damu za watu wanne waliofariki jana? stupidity.
 
Nadhani hili swala limewekwa kisiasa ili kutoua Trending Topics za nchi, na pia kutoshtua ujio wa ugeni wa Rais na wasindikazji wake kutoka sijui nchi gani ile. Walio kufa (kwa mujibu wa walioshuhudia, mimi nikiwa mmoja wapo) ni zaidi ya 40, almost basi zima na wengine wamefia Hospitali. Lakini vyombo vya habari vinatangaza tofauti, na watu wana-rely Media kupata habari bila kwenda kujionea Mochwari zilivyoshona mpaka mahospitali yanapeana Transfer.
Mkuu nafikiri kuna kitu hujakielewa kwenye tasnia ya habari,jukumu la media ku-report habari zisizokuwa na chembe ya mashaka,sasa lawama ambazo umezileta kwenye media siyo sahihi kwenye kutafuta habari kama hiyo unayoisema media imeandika taasisi husika imesema kwenda moncholi hii siyo kazi ya media na ndiyo maana utaona kuna quote kwenye hiyo habari na waliothibitisha ni mkuu wa polisi na mganga wa hosp hii inaitwa cross-checking na hao ndiyo source wa hiyo news.
 
Kuna vitu tunatakiwa kujiongeza,mleta mada nahisi nae alizimia kwenye ajali,media zote zimetangaza habari moja iliyotolewa na mganga mkuu wahospitali husika na kuthibitishwa na kamanda wa polisi,unataka waandike nn zaid au waseme lipi wasilo na uthibitisho nalo?
 
Kama kuna mtu aliangalia taarifa ya habari jana ITV unaweza kuonganisha dot ukajua hapa siasa imeingia, jana wakati wa taarifa ya habari yule mtangazaji alikwepa kabisa kutaja idadi ya watu akamuachia mkuu wa police ndo ataje ila ukiona body language ya mtangaza habari unajua kabisa hapa kuna siasa. Sijui huwa wanaficha nini? na hii ndo inapelekea kutochukuliwa hatua madhubuti ya kukomesha/kupunguza ajali za barabarani kwa sababu halionekani kama ni tatizo kubwa kwa sababu ukweli unafichwa sana.
Mkuu hakukwepa polisi ndiyo source kwenye ile story mwandishi anatakiwa kupata taarifa kwao/kwake hvy ili kuonyesha yakuwa amefanya kazi yake ipasavyo na ndiyo wenye jukumu la kuthibitisha sasa kama ni siasa ziko kwa hao polisi siyo media.
 
mimi nimekasirika sana kwa kweli kwa nini wamependelea kwenye kutoa taarifa... hawajatoa kabisa idadi ya ng'ombe zilizopoteza maisha na ngapi ni majeruhi na ziko wapi...............
yAANI WE ACHA TU...UTADHANI NA NG'OMBE NAO SIO WATU
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana, unajua nani anatakiwa kuthibitisha kifo? Unaweza kutofautisha mtu aliyezimia na aliyekufa kwenye ajali kwa kuangalia kwa macho? Na wale majeruhi waliotangazwa walienda kuokotwa kwenye ajali yingine? Sio kila ajali mnayoiona mbaya inaondoka na watu wengi. Fikiria kama umepita shule kidogo.
Hasipo kuelewa hapa basi tena. Hawezi kuelewa kabisa.
 
Back
Top Bottom