Habari za jioni wapendwa,
Nilikuwa ninatoka kwetu kijijini na vikapu vyangu vya ndizi na mihogo pamoja na mahindi. Nimepanda Raha Leo, njiani kama mtu simfahamu ninapenda kutumia ule muda kutafakari maisha yangu nikiwa nimefumba macho au ninasoma kitabu.
Siku hiyo nilipanda basi na mdada wa miaka kati ya 28-30, yule dada alikuwa na shauku ya kuongea na mimi, lakini nilichuna, mpaka tumefika Chalinze, alitaka miko na mimi nilikuwa nimekaa siti ya dirishani, ilibidi nivunje ukimya nilichukua pesa yake nikamchukulia miko na kumkabidhi mzigo na change yake.
Kutoka pale ni kama nilifungua tape, dada alitiririka, kuhusu ndoa yake, mama mkwe alivyo mchawi, mawifi wanaua watoto wake. Nilishukuru kuuchuna kutoka Tanga, Chalinze mpaka Ubungo si mbali sana.
Jamani hata kama kuongea kunapunguza stress, lakini tujue ya kuweka akiba. Kuna mwingine aliwahi kukutana na hali hii?